Nyenzo-rejea 2: Ulinganifu wa Magubike na Gairo

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Kijiji cha Mugaboke kinapatikana kilomita 5 kwenye barabara ya Morogoro

– Dodoma katika wilaya ya Kilosa ya Tanzania. Pamoja na kupata mvua ya uhakika na kutosha mwaka mzima, kijiji kimejaa chemchem .Wakazi wa kijiji cha Mugaboke ni wakulima mchanganyiko. Wanazalisha mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, viazi mviringo, ndizi na mboga za majani kama vile vitunguu, nyanya ,n.k .Pia wanafuga kuku, mbuzi na mifugo midogo midogo

Ingawa kimejaliwa rasilimali za asili za kutosha bado wakazi wa Mugaboke wana kiwango cha chini cha maisha. Wanapata bei ndogo kwa mazao yao ya kilimo, kwa vile wafanyabiashara hujihusisha na mkulima mmoja mmoja, badala ya kujihususha na vyama vya ushirika vya wazalishaji ambavyo wananchi walijaribu kuunda kwa kupitia wakala wa wafanyabiashara wadogo wa Agakhan. Kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulifikia soko, wanakijiji wanaweza kupata mahitaji ya msingi tu. Hawana uwezo wa kuzalisha rasilimali za kifedha ili kupambana na majukumu mengine ya kijamii kama vile vifaa vya kiafya, shule, maji ya bomba, nyumba za kisasa, umeme n.k

Gairo ni kituo cha kibiashara kwenye barabra kuu ya Morogoro - Dodoma. Kwa sababu ya kuwa kwenye njia ya usafiri ya kibiashara, wakazi wake kihistoria wameweza kujenga mawasiliano na miji mikubwa kupitia madereva wa malori. Pia wanajenga mtandao miongoni mwa madereva wa malori makubwa na wasafirishaji wengine, kunakowawezesha kusafirisha bidhaa zao kwa bei ndogo. Wakazi wengi wa Gairo ni wafanyabiashara. Wananunua mazao ya kilimo pamoja na kuku, mbuzi kutoka kwenye vijiji jirani kwa bei ndogo, na kuviuza kwa bei ya juu kwenye miji mikubwa kama vile Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam. Matokeo yake, wakazi wa Gairo wanaishi maisha ya kiwango cha juu ukilinganisha na watu wa vijiji vinavyowazunguka. Gairo ina huduma za kijamii kama vile zahanati, shule, umeme na maji ya bomba.

Nyenzo-rejea ya 1: Kuishi kwenye jamii tofauti

Nyenzo-rejea 3: Elimu kwa maendeleo Endelevu (EME)