Nyenzo-rejea 3: Elimu kwa maendeleo Endelevu (EME)

Taarifa za msingi/ ujuzi wa mada kwa mwalimu

Elimu kwa maendeleo endelevu ni nini?

‘Elimu kwa maendeleo endelevu inawezesha watu kujenga ufahamu, taratibu za maisha/maadili na ujuzi wa kushiriki kwenye maamuzi juu ya njia za kufanya mambo, mmoja mmoja au kwa pamoja, kitaifa na kimataifa, kuinua ubora wa maisha ya sasa bila kuharibu sayari kwa ajili ya siku zijazo?

(Kongamano la Elimu kwa Maendeleo Endelevu, 14 Septemba 1998).

Maendeleo endelevu ni sehemu muhimu ya uraia itakayowawezesha wanafunzi waweze:

  • Kufahamu kwamba pamoja na tofauti za kimaumbile, kivifaa na kiutamaduni kuna mengi yanayotuunganisha na dunia.
  • Kufikiri kwa makini na kuhoji kutokuwepo kwa haki na usawa;
  • Kuainisha, kuheshimu na kuthamini upana na mawazo anuwai;
  • Kujenga uhusika wa uwajibikaji kwenye masuala yanayohusu mazingira na maendeleo endelevu;
  • Kuwa tayari kwa matendo yao kuifanya dunia iwe mahali endelevu na penye usawa.
  • Kuwajibika kwa matendo yao.

Vyote, uraia na elimu ya maendeleo endelevu vinatoa fursa kubwa kwa namna nzuri ya kujifunza inayomlenga mwanafunzi ambayo mwanafunzi anapata hisia za kuwajibika kama raia wa dunia nzima. Mbinu hii ya kujifunza inajumuisha masomo yanoyochanganua sehemu mbali mbali za dunia na masuala yahusuyo mazingira. Kuchambua jamii zao na jamii nyingine za mbali kutawasaidia wanafunzi kupanua fikra zao kuhusu jinsi jamii na tamaduni tofauti zinavyokuwa; na jinsi tatizo linavyoweza kutatuliwa kwa njia nyingi tofauti; pia kupata mawazo mapya ya kupima na kujaribu. Elimu kwa maendeleo endelevu (EME) pia inaibua njia za kujitegemea zaidi. Hii inamaanisha kuwa unaweza kutumia vizuri rasilimali zinazokuzunguka lakini sio kuzitumia na kuzimaliza. Kufikiri njia za kurudishia au kupanda kutahakikisha uendelevu. Inamaanisha kutumia kile unachohitaji tu.

Rasilimali za kawaida si kwamba haziishi bali zina kikomo labda tujaribu kushirikiana na kuzitumia kwa busara na kuzirudishashia tunazotumia pale inapowezekana.

Imerekebishwa kutoka chanzo halisi: BBC World, Website

Nyenzo-rejea 2: Ulinganifu wa Magubike na Gairo