Somo la 1
Uanapotafiti familia ni muhimu kujua kwanza uelewa wa wanafunzi juu ya maana familia na kuwaonesha mipangilio tofauti ya familia. Kujua utofauti huu kunawasaidia wanafunzi kujisikia vizuri wanapotambua namna ambavyo familia zinaweza kutofautiana. Uchunguzi kifani 1 na shunguli 1 tunangali njia mbali mbali za kufanya hili.
Katika Uchunguzi kifani,mwalimu huwahamasisha wanafunzi kufanya kazi katika makundi madogo (rejea nyenzo muhimu: Utumiaji wa kazi za makundi katika darasa lako) na kukumbuka sheria walizokubaliana kufuata kwenye majadiliano ya vikundi.
Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia kundi dogo kutafiti familia yangu.
Bwana Nguzo, mwalimu wa Maarifa ya Jamii katika shule ya msingi Muhimu Tanzania alitaka wanafunzi wake wa darasa la tatu kujifunza kuhusu familia na kazi za familia mbalimbali.
Aliunda makundi ya wanafunzi wasiozidi sita. Aliwaweka wanafunzi pamoja ambao sio kawaida yao kufanya kazi pamoja.
Katika makundi wanafunzi walijibu maswali yafuatayo,ambayo ambayo mwalimu aliaandika ubaoni:
Jina lako nani?
Baba na mama yako ni nani? Taja majina yao
Babu na bibi yako ni nani? Taja majina yao
Una dada na kaka wangapi? Taja majina yao. Ni wakubwa au wadogo kuliko wewe?
Una binamu wangapi? Taja majina yao
Wakati wa majadiliano,Bwana Nguzo alikwenda kila kundi kuahakikisha kuwa wanafunzi wote walipewa nafasi ya kutoa mawazo. Baaada ya dakika
10 hadi 15,aliyataka makundi kushirikishana na darasa nini wametafiti kuhusu familia mbalimbali. Nini mfanano kati ya familia hizo? Nini totauti?(kwa wanafunzi wadogo au wasiojiamini huwauliza maswali zaidi, mfano: Nani alikuwa na kaka wengi?)
Pia aliyataka makundi kuzingatia swali hili.
Nini kinamfanya mtu awe dada ,kaka shangazi yako,n.k?
Baada ya dakika 10,mwanafunzi mmoja kutoka kila kundi huwasilisha majibu ya maswali la 6 darasani. Nguzo huandaa jedwali kubwa la mahusiano kusaidia kuongoza mjadala (Angalia Nyenzo rejea 1 jedwali la uhusiano )
Bwana Nguzo na wanafunzi wanajua kuwa ingawa kuna maneno katika lugha zao yanayoelezea kuhusu binamu, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa, mahusiano haya kwa kawaida hujulikana kama, kaka au dada, baba na mama. Kunautofauti kati ya kaka wa baba na kaka wa mama pia dada wa mama na dada wa baba. Mfano: Kaka wa mama ni mjomba lakini kaka wa baba ni baba mdogo/mkubwa; dada wa baba ni Shangazi lakini dada wa mama ni mama mdogo/mkubwa. Mwalimu Nguzo anagundua kwamba kufundisha wanafunzi kuhusu uhusiano wa kifamilia unaweza kuwachanganya wanafunzi wadogo.
Shughuli ya 1: Mimi ni nani?
Kabla ya kipindi, andaa jedwali la mahusiano (angalia Nyenzo rejea 1 )
Watake wanafunzi kufanya kazi katika makundi ya watatu au wane. Mwanafunzi mmoja ajitolee kuorodhesha watu wote anaowafahamu katika familia yake na kujaza habari zao kwenye jedwali la mahusiano (unaweza kumchagua mwanafunzi wewe mwenyewe)
Wanafunzi wanaweza kuhitaji kuchora picha za ndugu zao kwenye jedwali
Shirikishana majedwali haya na darasa lote
Jadili utofauti katika familia na sisitiza jinsi utofauti huo ulivyo mzuri
Mwishoni mwa kipindi, onesha jedwali la uhusiano kwenye ukuta wa darasa
Sehemu ya 1: Utafiti wa historia ya familia