Somo la 2
Tunapo jifunza mambo ya kale, ni muhimu kusaidia wanafunzi kuelewa kupita kwa wakati na jinsi vitu vinavyobadilika kutoka kizazi hadi kizazi.
Kubuni njia ambazo wanafunzi wanazitumia kujifunza historia za familia zao kunawasaidia kuhusianisha matukio pamoja na kuyaweka kwenye mtiririko mzuri. Nyenzo rejea 2: jedwali jingine la uhusiano linaonesha ukoo ambao utawasaidia wanafunzi kuona uhusiano kati ya wanafamilia mfano binamu yao ni mtoto wa dada au kaka wa mama au baba yao,
Uchunguzi kifani ya 2: Historia za familia
Juma Bhalo anapanga kufundisha wanafunzi wa darasa la tano kuhusu uhusiano wa kifamilia kwa kipindi fulani
Anakakata vipande kadhaa vya picha kutoka kwenye magazeti ya watu wa nyakati tofauti, wakifanya shughuli tofaut,:i mfano harusi, siku ya bonanza la shule, na kuandika namba nyuma ya kila picha. Aliwaambia wanafunzi wake kuwa picha zinawakilisha matukio tofauti kwa maisha ya mtu mmoja na kuwataka wanafunzi katika makundi ya watu sita kupanga picha kulingana na umri wake. Anawapa dakikia 15 kujadili mpangilio wao.
Halafu anawataka kila kundi kutoa mrejesho. Anawataka kueleza kwa nini walichagua mpangilio fulani na kuandika dondoo za picha zilizo wasaidia kupanga matukio. Wanajadiliana matukio muhimu yaliyoonyeshwa kwenye picha na Mwalimu Juma anawaambia wametengeneza kalenda ya matukio ya maisha.
Shughuli ya 2: Wanafunzi watengeneze kalenda zao za matukio
Nyenzo rejea 3: Kalenda yangu inaweza kuwa mwanzo kwa darasa kutengeneza kalenda yao ya matukio.
Kwanza, jadili umuhimu wa kujijua asili yako na wanafamilia wengine
Elezea maana ya kalenda ya matukio
Onyesha mfano kwa kutengeneza kalenda ya matukio yako mwenyewe (sio lazima utumie maisha yako halisi-unaweza ukatumia uhalisia wa maisha ya mtu fulani unaye mfahamu). Kuonyesha mfano ni njia muafaka ya kuwasaidia wanafunzi
kujifunza ujuzi mpya. Chora kalenda hii ubaoni waone na zungumzia nini unafanya au uwe umeiandaa kwenye karatasi kubwa. Kumbuka kutumia vipimo sahihi- mwaka uwakilishe na umbali fulani. (wanafunzi wako wanapotengeneza kalenda zao, watumie sentimeta za mraba 5 au umbali wa mkono kama hawana rula.
Watake wanafunzi kuandika vitu muhimu wanavyokummbuka kuhusu maisha yao. Pia wape muda wa kuwauliza wazazi/walezi kuhusu walipotembea kwa mara ya kwanza n.k.
Watake kunakiri taarifa yoyote wanayohitaji kuiweka katika kalenda ya matukio
Wasaidie wakati wanatengeneza kalenda zao. Unaweza kuwahamasisha kuandika matukio makubwa ambayo yamewatokea, na katika rangi tofauti.( au katika mabano chini ya mstari) matukio makubwa ambayo yalitokea katika familia zao( mfano dada mkubwa kwenda chuo, baba kununua shamba n.k)
Onyesha kalenda zao darasani
Wanafunzi wanaomaliza mapema wanaweza kuombwa kufikiri na kuchora kalenda ya muda ujao. Nini yatakuwa matukio makubwa wakati wana umri wa miaka 20,25,40 n.k?
Somo la 1