Somo la 3

Kusaidia wanafunzi kukuza ufahamu wao wa mambo ya zamani na sasa kunachukua muda, na inahusisha kuwapa kazi mbalimbali ambapo wanatakiwa kuona, kuuliza maswali na kufanya maamuzi kuhusu kile wanacho chunguza.

Wanawezaje kukuza ujuzi kuwasaidia kufikiri kuhusu namna vitu vinavyobadilika kulingana na muda? Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu unatumia mazingira ya kawaida kupanua ufahamu wa wanafunzi wako kuhusu muda unaopita na vitu vinavyobadilika.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutembelea mzee wa mahali

Mbwana Kato, Bibi Sime na Dada Benda waliandaa pamoja mafunzo ya jamii. Hawakufundisha wote mada moja kwa wakati mmoja, lakini iliwasaidia kushirikishana mawazo.

Wote walisoma Nyenzo muhimu: matumizi ya mazingira ya jamii/ mahali kama nyenzo. Walipanga kwenda pamoja na wanafunzi kutembelea wazee katika jamii kuongea nao kuhusu namna kijiji kilivyobadilika tangu walipokuwa watoto. Waliamua kugawa darasa katika makundi na kila kundi lingeandaa maswali ya kumuuliza mzee. Kila kundi lingeuliza maswali kwenye eneo tofauti kama michezo waliyocheza, chakula walicho kula,nyumba walizoishi n.k.

Shughuli muhimu: Matumizi ya vyanzo mbalimbali kuchunguza maisha ya zamani

Wape wanafunzi nafasi ya kutoa mawazo yao. Watake kufikiria jinsi wanavyoweza kuchunguza namna maisha yalivyobadilika katika familia zao, kijijini au katika jamii kwa kipindi fulani. Wangetumia nyenzo gani kuchunguza hilo?

Wanaweza kuwa na mawazo kama: kutumia uchunguzi na kumbukumbu zao kufikiri kuhusu nini kimebadilika katika maisha yao; kuuliza wazazi wao; kuzungumza na wazee wengine; kuongea na watu wenye mamlaka ( kama wafalme); kuangalia ramani za zamani; kutumia makumbusho (kama yapo); kusoma vitabu vinavyohusu eneo husika n.k.

Watake wanafunzi kukusanya hadithi kutoka kwenye familia zao kuhusu namna maisha yalivyobadilika kwa vizazi vichache vilivyopita, namna maisha ya kila siku yalivyokuwa. Zipi ni hadithi za zamani za familia zao? Je familia inachapisho lolote? Picha, barua.n.k zinazovyoonesha maisha yalikuwaje?

Wanafunzi washirikishane hadithi zao kwa kila mmoja darasani na tumia hadithi zao kama msingi wa mawasilisho –hii itajumuisha picha zinazoonyesha maisha yalivvokuwa,kazi zilizofanyika kwa maisha ya zamani maandishi yanayohusu hadithi za familia na nyaraka nyingine.na hadithi za kufikirika mfano: elezea siku moja katika maisha ya bibi yako wakati akiwa kijana.

Nyenzo-rejea ya 1: Jedwali la mahusiano/ukoo