Somo la 1
Kufundisha historia sio tu kunahusisha ukweli juu ya matukio ya kihistoria bali pia maendeleo ya ujuzi wa wanafunzi katika nyanja ya historia. Kama mwalimu, unatakiwa kuwapa wanafunzi wako nafasi ya kukuza na kufanyia mazoezi ujuzi huu. Aina ya matukio unayotafiti na wanafunzi wako yatategemea umri wao. Kwa watoto wadogo, utatoa mwongozo zaidi katika kuwasaidia kutafuta na kuelewa nini kilitokea.
Katika sehemu hii, wanafunzi watafanya mahojiano pamoja na waliowazidi umri katika familia zao au yeyote katika jamii. Lengo la mahojiano ni kutafuta namna wanavyotofautiana kimaisha, ukilinganisha na watu wa kale. Kwa kuwaonyesha wanafunzi namna ya kufanya mahojiano, unaweza saidia kukuza ujuzi muhimu-kuwa tayari kuona thamani ya historia simulizi na kuwa tayari kusikiliza. ( Rejea nyenzo 1: Historia simulizi ; kufahamu zaidi juu ya nyenzo hii muhimu)
Uchunguzi kifani 1 unaonesha namna mwalimu mmoja alivyowaelekeza wanafunzi wake wazo la kutumia historia simulizi kutafiti juu ya mambo ya kale. Soma hii na wanafunzi wako kabla ya kujaribu shughuli 1.
Uchunguzi kifani ya 1: Historia simulizi za familia
Kila mtu anahistoria yake. Bibi Eunice Shikongo, mwalimu wa darasa la tano katika shule ya Sheetheni nje ya Windhoek Namibia, hutaka wanafunzi wake kutafiti historia za familia zao kwa kumhoji mmoja wa wanafamilia.
Kwanza, hujadili maana ya ushahidi wa mapokeo kwa kuwahamasisha wanafunzi kushirikishana vitu walivyojifunza kutoka kwa wazazi wao. Huwauliza: Je, kile mlichojifunza kimeandikwa? Wengi wanakubali kuwa vitu walivyojifunza kwa njia hii havijaandikwa, lakini wameyapata kwa njia ya mdomo. Bibi Shikongo kisha huelezea kwamba, kwa kufanya mahojiano, wanafunzi watakusanya ushahidi wa mapokeo kuhusu zamani ilivyokuwa na watajua jinsi chanzo hiki kinavyoweza kuwa muhimu kuelezea mambo ya kale.
Huwasaidia kukusanya maswali muhimu watakayotumia kuwahoji wanafamilia zao (Angalia Nyenzo rejea 2: maswali yanayoweza kutumika katika mahojiano ). Halafu wanafunzi huongeza maswali yao kabla yakufanya mahojiano majumbani kwao.
Siku inayofuata, wanashirikishana matokeo ya utafiti na wanafunzi wenzao. Bibi Shikongo uandika muhtasari wa utafiti wao kwenye ubao kwa kichwa cha habari ‘Kale’. halafu, huwataka kujibu maswali yaleyale kuhusu maisha yao, na kuandika muhtasari wa maelezo yao chini ya kichwa cha habari cha habari, ‘Sasa’.
Huwataka kufikiri kuhusu namna maisha yao yanavyotofautiana na ya ndugu zao wa zamani. Halafu huwataka wanafunzi wawili wawili, kulinganisha Kale’ na ‘Sasa’
Wanafunzi wa umri mdogo huandika sentensi mbili/tatu kwa kutumia maneno ya ubaoni. Wanafunzi wakubwa huandika aya fupi.
Shughuli ya 1: Mahojiano ya ana kwa ana kuhusu utoto
Kwanza panga wanafunzi wawili wawili. Halafu, waambie wafikirie baadhi ya maswali wanayoweza kuuliza watu wazima kuhusu utoto wao. Wape wanafunzi muda wa kufikiri juu ya maswali yao na waambie muda watakaotumia katika zoezi
hili-yaweza kuwa siku mbili au tatu. Kama una wanafunzi wa umri mdogo, mnaweza kufanya pamoja kutengeneza maswali matatu au manne ambayo watakumbuka na kuweza kuuliza nyumbani.
Wakisha uliza maswali nyumbani, watake wanafunzi kushirikishana mawazo na wenzao.
Halafu, watake kila kundi la wanafunzi wawili kuungana na kundi lingine ili kushirikishana kile walichokipata.
Sasa waulize kila kundi la wanafunzi wanne kumalizia jedwali kuonyesha jinsi maisha yanavyoweza kubadilika.
Jadili na darasa lote namna maisha yalivyobadilika tangu wazazi wao na/au babu au watu wengine wa zamani walipokuwa watoto.
Uliza maswali yanayo wahamasisha kufikiri kwa nini mabadiliko haya yametokea.( Nyenzo muhimu: matumizi ya maswali kusaidia kufikiri inaweza kusaidia kufikiri aina gani ya maswali unahitaji kuuliza kuwahamasisha wanafunzi. Unaweza kuandika haya kabla ya kipindi kukukumbusha katika hatua hii.)
Tengeneza orodha ya mabadiliko ubaoni
Sehemu ya 2: Kutafiti namna tulivyoishi zamani