Somo la 2

Kama ulivyoweza kutumia historia simulizi kujua maisha ya kale, unaweza pia pamoja na wanafunzi wako kutumia kumbukumbu zilizoandikwa

Katika sehemu hii, tunaangalia namna jozi tofauti za kumbkumbu zinavyoweza kusaidia kujenga uelewa wao wa mambo ya kale. Katika shughuli 2 na shughuli muhimu , wanafunzi hutafiti kumbukumbu zilizoandikwa juu ya mambo ya kale na kufanya mahojiano ya ana kwa ana na wanajamii. Namna unavyoweza kutunga na kukusanya pamoja nyenzo ni sehemu ya jukumu lako. Ushauri unavyoweza kufanya kazi hii umetolewa.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia nyaraka kutafiti matukio yaliyopita.

Bwana Murungi ni mwalimu wa darasa la 6 katika Shule ya msingi Mkiwa, sehemu ya Marangu,

Tanzania. Siku ya kuhadhimisha uhuru wa Tanzania inakaribia na anataka wanafunzi wake kufikiri kuhusu historia ya Tanzania.

Alipeleka darasa lake maktaba ambako walisoma kuhusu matukio. Magazeti mawili, The Daily News na The Express , yamekwisha kuchapisha kuhusu uhuru na huwasomea wanafunzi sehemu ya machapisho kuamsha ari ya kutaka kujua. Vitinyi hivi vina historia ya maisha ya baadhi ya watu husika. Aligawa darasa lake katika makundi na kuwataka kila kundi kuchukua mmoja kati ya watu hawa na kujifunza habari zake,halafu kuandika historia ya yule mtu katika bango, kwa maonyesho katika ukumbi wa shule. Bango lazima lijumuishe namna walivyojihusisha na nini kimewatokea.

Wanafunzi wa Bwana Mrungi kisha walipanga kuonyesha matokeo ya utafiti wao kwa shule nzima. Mabango yao yalibandikwa kuzunguka ukumbi na baadhi ya wanafunzi walisimulia kwenye mkusanyiko wa shule nzima.

Nyenzo rejea 3: Uhuru wa Tanzania inatoa taarifa za msingi

Shughuli ya 2: Kujifunza tarehe muhimu katika historia.

Shughuli hii inategemea kutembelea sehemu za makumbusho, yaani makumbusho ya kitaifa ya Dares Salaam, lakini unaweza kutumia sehemu nyingine. (kama haiwezekani kutembelea makumbusho, unaweza kukusanya pamoja baadhi ya machapisho kwenye magazeti, picha na vitabu kusaidia wanafunzi wako kujitafutia wenyewe kuhusu tukio.

Chagua tukio fulani la kihistoria unalotaka wanafunzi wako walitafiti wakati wa kutembelea makumbusho (au darasani kama una nyenzo husika), mfano, harakati za ukombozi/uhuru. Ni muhimu kuzingatia ufahamu wa wanafunzi wako juu ya tukio fulani, hasahasa kama wanatembelea makumbusho yanayoonyesha matukio ya miaka mingi iliyopita.

Gawanya wanafunzi kwenye makundi, ukiwapa kila kikundi mada tofauti ya kuzingatia juu ya tukio la kihistoria 

Jadili aina ya maswali wanayoweza kuhitaji kutafutia majibu wakati wakisoma na kuangalia maonyesho (kama ni kwenye makumbusho) au nyenzo (kama ni shuleni).

Darasani, watake wanafunzi kwenye makundi yao kuandika juu ya utafiti wao katika mabango makubwa. Yaweke mabango darasani au ukumbini kwa wote kuona.