Somo la 3
Sehemu hii inalenga kupanua mawazo yako namna ya kusaidia wanafunzi kutumia historia simulizi kama nyenzo ya kujifunzia juu ya mambo ya kale. Utawahamasisha kufikiri kiundani juu ya ukweli na uhalisia wa ushahidi huu, na kulinganisha ushahidi wa mapokeo ya matukio ya kihistoria pamoja na ushahidi wa maandishi kwa tukio hilohilo. Kutafiti ufanano na utofauti katika aina mbili za ushahidi kunatoa nafasi nzuri kwa wanafunzi kujifunza.
Uchunguzi kifani ya 3: Kukusanya ushahidi wa mapokeo
Bi Paka Ngowa hufundisha historia darasa la Sita kwenye shule ndogo nje kidogo ya Dares Salaam, Tanzania. Familia nyingi katika eneo hilo zilihusika kwenye matukio yaliyopelekea kupatikana kwa uhuru wa Tanzania. Bi Ngowa amewaarika shuleni wageni wawili walioshiriki katika harakati za kupata uhuru ili kuelezea juu ya uzoefu wao. (angalia
nyenzo rejea muhimu: kutumia jamii/mazingira husik a kama nyenzo zitakazo kusaidia kuandaa na kupanga ujio huo) Watakuja kwa siku mfululizo kwa vile hawajuani na wana mitazamo tofauti juu ya uhuru wa Tanzania.
Bi ngowa huwatahadharisha wanafunzi kwamba watu hawa wawili kwa sasa ni wazee sana, na kumbukumbu zao sio nzuri muda wote. Kabla ya wageni kufika, wanafunzi huandaa baadhi ya maswali muhimu wanayotaka kuuliza kwa wazee hao. Kwa siku mbili, wageni hufika na kusimulia hadithi zao. Wanapoondoka, Bi Ngowa na wanafunzi hujadili ufanano na tofauti kati ya hadithi mbili. Pia hujadili sababu zilizopelekea kutofautiana.
Mwalimu huorodhesha dondoo muhimu zilizojitokeza kwenye hadithi zao. Pia huelezea kwamba ingawa historia simulizi inaweza kufanya wanafunzi waelewe vizuri uhuru wa Tanzania, lakini mara nyingine wasimuliaji hawawezi kuwa sahihi na hadithi za watu tofauti huweza kutofautiana. Bi Ngowa anaamini kuwa wanafunzi wake wamejifunza kipindi muhimu katika matumizi na matatizo ya historia simulizi.
Shughuli muhimu: Kulinganisha mahojiano na nyaraka zilizoandikwa
Pamoja na wanafunzi wako, taja tukio muhimu la kihistoria (kama mapigano ya kikabila, au uasi) yaliyotokea. Kama unaweza, tafuta nyaraka zilizoandika juu ya hilo.
Katika kuandaa shughuli hii, unahitaji kujua (kama mwalimu) kuhusu kile jamii yako inachofahamu juu ya uasi au tukio husika. Kumbukumbu hizi ni hadithi simulizi iliyorithiwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watambue baadhi ya watu muhimu ambao wanafunzi wako wanaweza kuzungumza nao nyumbani au wanaweza kuja shuleni.
Peleka wanafunzi wako nje kwenye makundi kwa mahojiano/usaili na wazee hawa. Watake wanafunzi kuorodhesha dondoo muhimu kumi zilizotolewa na kila mhojiwa/msailiwa (Hakikisha wanafunzi wanakwenda kimakundi tu na wako salama muda wote.)
Mkirudi darasani, watake wanafunzi kuelezea matokeo muhimu ya utafiti.
Watake kila kundi kubuni chati/bango la tukio husika, ikijumuisha matukio muhimu na kutumia baadhi ya maelezo ya wageni kutoa hisia ya kile kilichokuwepo.
Onyesha hii darasani.
Jadili pamoja na wanafunzi wako kama wanafikiri wanaushahidi wa kutosha juu ya nini kilitokea kutoka kwa watu walio zungumza nao. Kama hakuna, namna gani wanaweza kutafiti zaidi?
Somo la 2