Nyenzo-rejea ya 1: Historia simulizi
Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi
Wote tunahadithi za kusimulia, hadithi kuhusu maisha yetu na matukio muhimu yaliyotokea. Tunatoa uzoefu wetu na kuunganisha kumbukumbu zetu kufanya ziwe hadithi. Hadithi hizi zinaweza kuturuhusu kujenga picha halisi juu ya nini kilitokea kama zitaunganishwa na kumbukumbu za watu wengine katika tukio moja.
Jamii yako itakuwa chanzo muhimu kwa utafiti wa nini kilitokea kwa tukio husika au nini kinahisiwa kuwepo pale miaka 20 iliyopita. Wanafunzi wako wanaweza kutafiti vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Wanigeria au vita vya Biafra au matukio mengine.
Nini maana ya historia simulizi?
Historia simulizi siyo uwongo au uvumi lakini ni historia ya kweli ya watu wanaozungumziwa kutokana na mitazamo yao kadili wanavyoikumbuka. Inahusu mpangilio mzuri wa ukusanyaji wa hadithi juu ya uzoefu wa
watu. Kumbukumbu hizi za kila siku zina umuhimu kihistoria. Zinatusaidia kuelewa maisha jinsi yalivyo. Kama hatukusanyi na kuzitunza kumbukumbu hizo, siku moja zitapotea moja kwa moja.
Hadithi zako na hadithi za watu wanaokuzunguka ni za pekee na zinaweza kukupa taarifa muhimu.
Kwa sababu tunaishi kwa miaka kadhaa tunaweza kuwa na kumbukumbu za kipindi tu cha maisha. Hii
hufanya wanahistoria wawe na wasiwasi kwamba wanaweza kupoteza kumbukumbu muhimu na mitazamo juu ya matukio. Kukusanya hadithi hizi husaidia wanafunzi wako kukuza hisia za kujitambua wao wenyewe na namna gani wanajiweka katika hadithi ya mazingira yao.
Namna gani unakusanya hadithi za watu?
Unapokuwa umeamua ni tukio au shughuli gani unataka kuichunguza, unahitaji kutafuta watu waliohusika na kuwaomba kama wapo tayari kukusimulia hadithi zao.
Wasiliana nao kupanga muda na waambie nini unataka kuzungumzia na nini utafanya.
Unahitaji kunukuu wanachokisema. Unaweza kufanya hivyo kwa kuandika kwa mkono au ikiwezekana kwa kuchukua mkanda wa video au kurekodi sauti.
Baada ya kukusanya habari au ushahidi wao, ni muhimu kulinganisha na kutofautisha mitazamo ya watu tofauti kwenye tukio hilohilo, ili kuweza kugundua ukweli kutoka tafsiri za watu mbalimbali walizonazo juu ya tukio hilo. Unaweza kuwaomba wanafunzi wako katika makundi kufanya mahojiano na watu mbalinbali na halafu kuandika ufupisho wa utafiti wao ili kushirikishana au kushirikiana na wanafunzi wengine. Kitabu kinaweza kutengenezwa kuhusu utafiti wa wanafunzi juu ya tukio Fulani.
Imenukuliwa kutoka Do History, Website
Somo la 3