Nyenzo-rejea ya 3: Uhuru wa Tanzania
Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi
Tanganyika ilipata uhuru kamili tarehe 9 Desemba 1961 baada ya Nyerere kuwa Waziri Mkuu mapema mwaka huo. Hatukumwaga damu. Huu ulikuwa mfano mzuri wa kile kinachofanywa na umoja na mshikamano na pia ulikuwa mwanzo mzuri kwa taifa. Uhuru wa Zanzibar haukuja kirahisi, ingawa walikuwa chini ya Waingereza, Waarabu walitawala kikamilifu na wao pia walihitaji uhuru. Ukijumuisha kutokubaliana kati ya Waasia,Waafrika na Waarabu wenyewe, utakuwa huna njia nyingine zaidi ya mapinduzi-na ndicho hicho kilichotokea. Baada ya miaka miwili ya kukosa utulivu-na katika jitihada za kuongeza mchakato wa kujitawala- PAFM( Pan African Freedom Movement) kwa Africka Mashariki, Kati na Afrika Kusini viliunganisha vyama vya upinzani na mwaka 1963 mwezi wa Sita, uhuru ulipatikana.
Uhuru kamili wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza ulitolewa tarehe 10
Desemba 1963. kulifuata kutoridhika, na Januari 1964 baada ya vurugu na vita vya wenywewe, Sultani na serikali yake walifukuzwa. Msukumo mkubwa wa mapinduzi ulitoka chama muhimu cha UMMA, chini ya uongozi wa Abdul Rahman Mohammed,kwa kushirikiana na John Okello wa Kenya. Tarehe 11 Januari 1964 walitwaa Zanzibar Mjini na kutangaza serikali mpya ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tarehe 26 Aprili 1964 Zanzibar, Pemba,na Tanganyika ziliungana kufanya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kama sehemu ya katiba, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ingebaki na uhuru na Raisi wake angekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tanzania ilipopata uhuru wake, ilikuwa masikini na nchi ya mwisho kimaendeleo kwa Afrika Mashariki. Nyerere alikuwa na wasiwasi kuwa wale waliokuwa madarakani wangejitajirisha wenyewe kwa gharama za watu masikini waishio vijijini na kuzuia hilo, alifanya Tanzania iwe na mfumo wa chama kimoja na siasa ya ujamaa. Hili halikuwafurahisha viongozi wa Magharibi. Nyerere alizungumzia upinzani dhidi ya utawala uliojitangazia uhuru Rhodesia, alipata upinzani kutoka kwa Waingereza ambao walikata misaada yote kwa Tanzania. Msaada wa Nyerere kwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Msumbiji na Angola pia uliiongezea Tanzania maadui hasahasa alipowaruhusu ANC na FRELIMO kufanya shughuli zao Tanzania.
Tanzania pia ilivamiwa na Idi Amin –kiongozi wa Uganda maarufu kwa utawala wake wa mauaji-wakati Nyerere alipowahifadhi baadhi ya Waganda pamoja na Milton Obote na Yoweri Mseveni. Amin alivamia kaskazini magharibi mwa Tanzania Oktoba 1978 na kulilipua Bukoba na Musoma. Mwaka 1979, Nyerere aliweka pamoja jeshi dogo la Tanzania na kujibu kwa kuvamia Uganda na kumwondoa Amin madarakani. Moja kwa moja kitendo hicho kililaaniwa na viongozi wengine wa Afrika-mbali kwamba Amin alikuwa mchokozi. Pia vita hiyo ilishusha uchumi wa Tanzania kwa vile hakukuwa na fidia-iwe kutoka Magharibi au sehemu nyingine ya Afrika.
Wakati huohuo, Zanzibar, mambo yalikuwa hayajatulia. Zanzibar hawakukubali kuungana na Tanganyika matokeo vurugu ziliendelea. Abeid Karume, raisi wa kwanza wa Zanzibar aliuwawa mwaka 1972 na nafasi yake ilichukuliwa na Abdu Jumbe. Miaka michache baadae katika harakati kutuliza vurugu kutokana na kuungana kwa Tanzania bara na Zanzibar, Nyerere aliamuru kuundwa nchi ya chama kimoja kilichoitwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Muungano uliridhiwa Aprili 1977 na ingawa leo kuna chaguzi za vyama vingi, CCM imebaki chama chenye nguvu katika siasa za Tanzania.
Imetolewa kutoka Absolute Tanzania, Website
Nyenzo-rejea ya 2: Maswali yanayoweza kutumika kwenye mahojiano