Somo la 1

Kwa kuangalia mazingira ya kawaida na muundo wa nchi inawezekana kufiria sababu zilizofanya jamii kukaa mahali Fulani.

Zimbabwe kuu ni mfano mzuri. Kama mwalimu wa mafunzo ya jamii nimuhimu kuelewa kifani kama hiki, ambacho kinakupa ujuzi wa kuhusianisha mawazo haya na falme tofauti za Kiafrika pamoja na mazingira yako halisi. Kutumia ziara za mafunzo kama ziara kwenye eneo fulani huwezesha kujionea wenyewe kwanini sehemu moja ilichaguliwa kwa makazi na kwanini baadhi ya maendeleo yamedumu kwa muda mrefu kuliko mengine.

Makazi mengi yapo pale kwa sababu mazingira yana baadhi ya mahitaji muhimu kama vile maji au miti, na/au eneo linatoa ulinzi kutoka vitu fulani au dhidi ya maadui. Vijiji na miji mara nyingi hupatikana jirani na mito au misitu ambayo hutoa maji na miti ya ujenzi na kuni. Kwa kuangalia kwa ukaribu mazingira ya shule yako au nyumbani kwa wanafunzi, utawasaidia kuelewa jinsi makazi yalivyoanzishwa.

Ramani za zamani zitaonyesha jinsi eneo lilivyobadilika muda hadi muda (hii inaweza kuwa mwendelezo wa shughuli za matembezi kutoka moduli 2, Sehemu 1).

Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza maeneo ya utamaduni.

Sekai Chiwamdamira hufundisha darasa la sita katika shule ya msingi Musvingo Zimbabwe. Shule yake iko karibu na eneo la utamaduni la Zimbabwe kuu. Anafahamu kuwa wanafunzi wake wengi pindi waendapo shuleni hupita karibu na eneo hili maarufu lililozungukwa na kuta za mawe. Lakini haelewi kama wanajua kwa nini lipo pale. Sekai hutaka kuwasaidia wanafunzi kutambua kwamba ardhi na rasilimali zake za asili zilichangia katika uamuzi wa watu kuishi katika Zimbabwe Kuu.

Alianza kipindi kwa kuelezea jinsi Zimbabwe kuu ilivyokuwa na nguvu katika falme za kiafrika ambayo ilikuwepo miaka ya 1300-1450 ( rejea nyenzo 1: Zimbabwe kuu ). Huwataka wanafunzi kufikiria kwa nini watawala wa falme hii walichagua kuishi katika miinuko ya Zimbabwe kuliko eneo lingine katika Afrika. Ramani ni nyenzo yake muhimu kwa majadiliano haya ( rejea nyenzo 2: ramani ya picha ya Zimbabwe kuu

). Huonesha uwepo wa dhahabu pembe za ndovu, mbungo, uwepo wa maji na njia za kibiashara kwenye ramani: huwataka wanafunzi wake kupendekeza namna kila moja ilivyochochea watu kujenga makazi hapo yalipo. Kadili wanafunzi wanavyotoa mapendekezo yao, Sekai huchora picha ya mawazo ubaoni

Sekai ameridhishwa na kiwango cha kufikiri na majadiliano kilichoonyeshwa.

Shughuli ya 1: Kutumia ramani kupata taarifa kuhusu Zimbabwe kuu

Kabla ya kipindi, nakiri ramani na maswali kutoka nyenzo ya 2

kwenye ubao au andaa nakala kwa kila kikundi.

Kwanza, elezea kile kinachowakilishwa na ufunguo ubaoni. Halafu, gawanya darasa katika makundi na kitake kila kikundi kupambanua ufunguo kuhusiana na ramani ya Zimbabwe kuu. Kubali kila kitu kinachowakilishwa na ufunguo.

Uliza wanafunzi wako kwanini wanafikiri waliishi hapa kwanza. Unaweza kutumia maswali kutoka nyenzo ya 2 kama msaada kuanza majadiliano.

Kadili unavyofanya, zunguka zunguka katika makundi kutoa msaada pale unapohitajika kwa kuuliza maswali yanayowaongoza.

Baada ya dakika 15, kitake kila kikundi kuorodhesha mawazo yao

Baada ya hapo, watake kupanga mawazo yao kulingana na umuhimu wake.

Andika mawazo yao ubaoni

Mwisho, waambie wanafunzi kupigia kura sababu tatu wanazofikiri ni muhimu.

Kwa watoto wadogo, unaweza kuangalia katika vitu katika mazingira yao na watake wafikiri kwanini binadamu walishi hapa.

Sehemu ya 3: Kutumia njia tofauti za ushahidi katika historia