Nyenzo-rejea ya 4: Ng’ombe na utamaduni wa maisha ya Wamasai.
Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.
Maisha ya kabila la wamasai waishio Kenya na Tanzania yanahusu ng’ombe wao ambao ni chanzo kikuu cha chakula na uchumi wao. Wanaamini kuwa Mungu aliwapa ng’ombe wakuchunga na majukumu ya kijamii na hadhi yao inapatikana na mahusiano yao na ng’ombe.
Madaraja ya Wamasai hutegemea kiasi cha ng’ombe ilichonacho familia, hivyo ng’ombe ni mara chache huchinjwa; huachwa wazaliane kama ishara ya utajiri na huuzwa au kununuliwa kulipa deni. Mara nyingine askari wa kimasai huandaliwa kimakundi kwa lengo la kuiba au kunyang’anya ng’ombe.
Mazingira yao ya kuchungia ngombe yanaanzia katikati ya Kenya hadi katikati ya Tanzania. Vijana wakiume wanahusika kuchunga ng’ombe na kawaida huishi kwenye kambi ndogondogo, wakihama mara kwa mara kutafuta maji na malisho mazuri. Kwa vile wanahamahama, Wamasai hujenga nyumba za muda kwa kinyesi cha ng’mbe na matope. Mchanganyiko huu hukauka haraka na jua na ni mgumu kama saruji na hautoi harufu. Nyumba hujengwa kwa mduara; usiku ng’ombe wote huwekwa katikati ili kuwaepusha na wanyama wakali.
Maziwa ya ng’ombe pamoja na damu ni chakula cha kila siku kwa wamasai ambao hawali matunda wala nafaka. Mara moja kwa mwezi damu huchukuliwa kwa wanyama hai kwa kuchoma mkuki shingoni.
Damu hii huchanganywa na maziwa kwenye kibuyu kilichooshwa kwa mkojo kuzuia yasiharibike.
Imenukuliwa kutoka: University of Iowa, Website
Nyenzo-rejea ya 3: Ufahamu juu ya ufugaji ngo’mbe