Sehemu ya 4: Ufahamu wa Chati ya kalenda ya matukio
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia kalenda ya matukio ya kihistoria na nyenzo nyingine kukuza ufahamu wa chanzo na matokeo?
Maneno muhimu: Chati ya wakati na matukio, mabadiliko ya kihistoria; mpangilio wa matukio ya kihistoria; historia; vyanzo vya kihistoria; mdahalo
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- umetumia kalenda ya matukio kuonyesha mabadiliko ya kihistoria kipindi hadi kipindi;
- umewasaidia wanafunzi kutambua matukio muhimu katika mchakato fulani wa kihistoria;
- umewahamasisha wanafunzi kuiangalia historia sio kama mtiririko wa tarehe za kujifunza lakini ni mchakato wa kutafiti;
- Umetumia nyenzo mbalimbali kusaidia wanafunzi kujifunza kwamba tukio moja linaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi.
Utangulizi
Unapokuza ufahamu wa muda uliopita na unaoendelea kupita, ni muhimu kuwa na uwezo wa kupanga matukio katika mpangilio fulani kulingana na yalivyokuwa yanatokea.
Mara nyingi wanafunzi huhangaikia kujua dhana ya muda. Katika sehemu hii kitu cha kwanza utawasaidia wanafunzi wako kugawanya muda katika vipindi ambavyo ni rahisi kuelewa; mara wakiweza kufanya hili, kufikiri kuhusu mtiririko wa matukio na kwa nini ni muhimu. (kwa wanafunzi wadogo hili linaweza kurahisishwa kwa utawasaidia namna ya kupanga kazi fulani wanazozifanya, ukiwaelekeza kwenye shughuli ngumu kadili ufahamu wao unavyoongezeka). Utawasaidia wanafunzi wako kutambua matukio muhimu katika kipindi fulani. Hili litawaongoza wanafunzi wadogo na wakubwa kwenye uchambuzi wa chanzo na matokeo yake, na kujua kuwa kuna sababu zaidi ya moja katika tukio fulani.
Nyenzo-rejea ya 5: Umuhimu wa ng’ombe-zamani na sasa.