Somo la 1

Kutafiti kipindi fulani cha kihistoria, na kujaribu kupanga matukio kwa mtirirko kadili yalivyotokea kutasaidia wanafunzi kuanza kuona uhusiano kati ya matukio na baadhi ya sababu za matukio. Kujua chanzo cha mabadiliko katika nchi na jamii zetu, inaweza kutusaidia kuishi maisha bora.

Kusudio la sehemu hii ni kutafuta namna matumizi ya kalenda ya matukio ya kihistoria yanavyoweza kuwa ni njia muhimu katika kugawanya vipindi ili kujua ni kipindi gani tunahusika nacho. Hili ni muhimu hasa pale tunapofundisha historia kwa sababu ni lazima wanafunzi kujua mabadiliko kutegemeana na muda.

Wanafunzi wanahitaji kusaidiwa kuchambua na kupanga matukio kutoka utotoni. Kadili wanavyokua na kuishi wanaweza kurejea shughuli kama hizi kwa kutumia mchanganyiko zaidi wa matukio.

(Sehemu ya 1 katika moduli hii imetumia kalenda ya matukio kutafiti historia ya familia. Inafaa kuangalia sehemu hiyo kama bado hujapitia, hasa kama unafanya kazi na wanafunzi wenye umri mdogo)

Uchunguzi kifani ya 1: Mpangilio wa matukio

Tetha Rugenza, ambaye hufundisha historia katika shule ndogo Rwanda, anataka kuwaonyesha wanafunzi wa darasala 4 jinsi ya kugawanya muda katika vipindi vidogo vidogo. Ili kufanya hili, huandaa kipindi ambapo wanafunzi na yeye mwenyewe hujifunza namna ya kutengeneza kalenda ya matukio na kuigawanya katika vipindi.

Rugenza huamua kutumia mfano wa Rwanda. Huchora kalenda ya matukio ya historia ya Rwanda ubaoni. Kuwasaidia wanafunzi kuelewa dhana ya vipindi, hugawanya historia ya Rwanda katika vipindi vya kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na wakati wa uhuru.

Huandika orodha ya matukio muhimu pamoja na tarehe yalipotokea kwenye vipande tofauti vya karatasi na kuweka mezani. Kila tukio, analowaelezea wanafunzi lipo katika kipindi fulani. Huwataka wanafunzi wake kupanga matukio kulingana na vipindi yalipotokea.

Huanza na tukio moja na huruhusu mwanafunzi kuchukua tukio la pili na kubandika sehemu husika kwenye kalenda ya matukio. Wanafunzi wengine huhakikisha kama tukio limewekwa katika sehemu sahihi. Kupitia majadiliano, huwasaidia wanafunzi kama hawana uhakika na mahali tukio linapotakiwa kuwekwa. Huwataka wanafunzi kufikiri kama kuna matukio mengine ya kitaifa yanayoweza kuwekwa kwenye kalenda ya matukio nayo pia huyapanga katika mtiririko unaofaa.

Shughuli ya 1: Uchoraji wa kalenda ya matukio

Waambie wanafunzi kuwa wanatakiwa kutengeneza kalenda ya matukio ya shule kwa pamoja.

Anza kipindi kwa kuwataka wanafunzi wako kuandika matukio muhimu yaliyotokea shuleni katika mwaka husika.

Watake wanafunzi kutoa tarehe ya kila tukio kama wanaweza au watafute tarehe hizo.

Watake wanafunzi kupanga matukio haya kutoka mwanzo hadi mwisho wa mwaka wa shule.

Wasaidie wanafunzi kufanya uamuzi kuhusu ukubwa wa kalenda za matulio wanaoutaka na kutengezeza kipimo inavyotakiwa.

Watake wanafunzi kuonyesha mwezi kwa usahihi kulingana na vipimo walivyochagua na kuandika tarehe za matukio kushoto mwa kalenda- matukio ya miaka ya zamani yaanzie chini nay a tarehe za karibuni yawe juu.

Katika upande wa kulia wa kalenda ya matukio, watake wanafunzi waandike maelezo mafupi ya tukio husika dhidi ya kila tarehe.

Weka wazi hiyo kalenda ili wote waione. (kama huna nyenzo za kutosha kwa kila mwanafunzi kufanya peke yake, basi kazi hii inaweza kufanywa katika makundi ya wanafunzi wasiozidi watano.) Darasa zima wajadili kama kuna matukio ya shule yaliyoweza kutokea wakati wowote katika mwaka. Je kuna yale yanayotokea katika kipindi fulani? Kwa nini? (kwa mfano, kwa nini mitihani ya kumaliza mwaka haiwezi kufanywa mwanzoni mwa muhula?

Zamani, ng’ombe walitazamwa kama rasilimali muhimu, na wakulima wengi na jamii bado hutazama ng’ombe katika mtazamo huu.

Sehemu ya 4: Ufahamu wa Chati ya kalenda ya matukio