Somo la 2
Lengo la shughuli ya 2 ni kwa wanafunzi kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika jamii za Kiafrika kwa kutumia jamii husika kama chanzo cha taarifa. Hapo wanafunzi watagundua kiasi gani jamii za wakulima zimebadilika.
Uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 , tumia akili na mwongozo kusaidia wanafunzi juu ya shughuli hii kadili wanavyoshirikiana katika makundi.
Uchunguzi kifani ya 2: Shughuli za kilimo Arusha
Kuna wakulima wengi wanaoishi Arusha na wengi wa wanafunzi mashuleni ni watoto wa wakulima.Wema pamoja na wanaunzi wake wanataka kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika maisha na utamaduni wa wakulima wa zamani walioishi Tanzania.
Wema huanza kipindi chake kwa kuelezea jukumu muhimu la ng’ombe katika jamii za Kiafrika siku hizo. Huchora ramani ubaoni ambayo husisitiza umuhimu wa ng’ombe na namna ng’ombe walivyotumika. ( Nyenzo rejea muhimu: Kutumia picha ya mawazo na majadiliano na
Nyenzo 3: ufahamu kuhusu ufugaji ng’ombe kukusaidia kuwauliza maswali wanafunzi). Wanafunzi wajadili mawazo hayo
Katika kipindi kijacho, mtu mzima na wanafunzi katika makundi watakwenda kuwauliza maswali wakulima. Wema amewasiliana nao kujua ambaye yupo tayari kuongea na wanafunzi.
Wanafunzi walikuwa na maswali rahisi mawili ya kuwauliza wakulima
Kwanini ng’ombe ni muhimu kwako? Nini matumizi ya ng’ombe?
Darasani, wanafunzi hushirikishana utafiti wao na Wema huorodhesha majibu yao ubaoni. Wanajadiliana juu ya kile kilichobadilika kulingana na wakati.
Shughuli ya 2: Kilimo cha zamani na sasa.
Kabla ya kipindi, soma nyenzo 4: Ng’ombe katika maisha ya kitamaduni-Wamasai.
Elezea kwa wanafunzi umuhimu wa ng’ombe kwa watu wanaoishi Tanzania
Wakiwa katika makundi , watake kuorodhesha sababu zilizopelekea wafuge ngombe
Kwa kazi ya nyumbani, waombe kutafiti kutoka kwa wazee wa jamii zao namna ufugaji ulivyobadilika.
Katika kipindi kinachofuata, waombe wanafunzi kunakiri na halafu kujaza mwongozo katika Nyenzo 5: Umuhimu wa ng’ombe –zamani na sasa kudondoa mawazo yao.
Shirikishana na wanafunzi wote majibu ya kila kundi na weka mwongozo ukutani kwa siku kadhaa ili wanafunzi waweze kujikumbusha.
Somo la 1