Somo la 3
Njia mojawapo ya kujua jinsi jamii ya kale ilivyoishi ni kuchunguza majengo, kazi za sanaa, sanamu na alama za muda mrefu zinazopatikana sehemu fulani.
Katika sehemu hii, wanafunzi waende ziara kwenye maeneo ya kihistoria. Kama hili haliwezekani kwa darasa lako, inawezekana kufanya jambo linalofanana na hilo darasani kwa kutumia nyaraka mbalimbali, picha na kazi za sanaa. Wanafunzi wanaweza kuelewa jinsi ya kutafiti hili na kujaza baadhi ya nafasi wenyewe kuhusiana na nini kilitokea.
Uchunguzi kifani ya 3: Uandaaji wa ziara ya mafunzo
Jasmin ameshafanya uchunguzi na wanafunzi wake wa darasa la tano kuwa huenda mwanzo wa binadamu ni Afrika Mashariki. Sasa anawataka kufikiri jinsi tunavyojua juu ya hili, kwa vile shule yake ipo jirani na makummbusho ya Olduvai Gorge yaliyo Ngorongoro, huandaa ziara ya mafunzo. Hutaka wanafunzi kuchunguza kazi za sanaa na picha, na kufikiri jinsi wanahistoria walivyotumia taarifa kuongeza uelewa wetu juu ya mabadiliko ya mwanadamu.
Ziarani, wanafunzi wachukue dondoo za taarifa kwenye chati na picha. Pia wanaelezea na kuchora baadhi ya kazi za sanaa na alama ambazo zipo Olduvai Gorge.
Shuleni, hujadili vitu vyote walivyoona na kusikia na kuviorodhesha ubaoni. Jasmine huwaomba kupanga tafiti zao chini ya vichwa tofauti vya habari juu ya aina za majengo waliyoona. Halafu wanafunzi hujadili wanachofikiri kuhusu matumizi ya majengo, kwa kuzingatia mwonekano wake na kazi za sanaa na sanamu zilizomo. Jasmin husaidia kujaza nafasi kwa kuelezea maana ya baadhi ya kazi za sanaa na sanamu. Mawazo hutolewa na wanafunzi wengine wanaalikwa kuona kazi yao.
Rejea Nyenzo muhimu: matumizi ya mazingira ya asili/jamii husika kama nyenzo muhimu
Shughuli muhimu: Kutafiti historia ya mahali
Kabla hujaanza shughuli hii, kusanya taarifa za kutosha kadili unavyoweza kuhusu jamii ya mahali kama ilivyokuwa. Unaweza kuwa na machapisho ya magazeti, dondoo za mazungumzo na wazee katika jamii hiyo, majina ya watu waliotayari kuongea na wanafunzi wako.
Panga wanafunzi kwenye makundi. Elezea kuwa watatafiti kuhusu historia ya kijiji kwa kutumia nyenzo mbalimbali. Kila kundi litashughulika na kipengele kimojawapo, kwa mfano duka, kanisa au shule.
Angalia nyenzo ulizonazo, kabla hujaenda kuongea na watu.
Wape wanafunzi muda wakuandaa maswali na halafu wapangie siku ya kwenda kuuliza maswali kuhusu kipengele chao.
Warudipo shuleni, kila kundi liamue namna ya kuwasilisha utafiti wao darasani.
Shirikishana utafiti
Unaweza kutoa kitabu cha kazi zao kuhusu historia ya eneo husika.
Somo la 2