Nyenzo-rejea ya 3: Matukio muhimu kuelekea uhuru
Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi
1957 | Ghana inakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kupata uhuru chini ya Kwame Nkrumah kupitia mikutano kama ile ya Ghandi, migomo, kuwalazimisha Waingereza kutoa uhuru |
1958 | Chinua Achebe(Nigeria): Things Fall Apart, kilicho andikwa kwa ‘Kingereza cha Kiafrika’ kinachunguzia madhara ya utamaduni wa Magharibi kwa tamaduni za asili. |
1958 | Mkutano wa mataifa yote ya Afrika: suluhisho la ubepari na ukolini, Accra, 5-13 Desemba 1958 |
1954–1962 | Makoloni ya Kifaransa (mataifa ya Kiafrika yanayo zungumza Kifaransa) yanakataa kuendelea kutawaliwa hata kama wanatambua kuwa uchumi na tamaduni zao bado zinategemea Ufaransa-isipokuwa Algeria iliyokua na walowezi wapatao millioni 1. Vita vya kikabila nchini Algeria viliendelea hadi ulipopatikana uhuru mwaka 1962, miaka sita baadae baadaye Moroko na Tunisia kupata uhuru. |
1958 | Makaburu wenye asili ya Kidachi walipata uhuru kutoka kwa Waingereza Afrika Kusini. |
1964 | Nelson Mandela, katika hukumu ya uhaini na viongozi wenzake wa ANC mbele ya Mahakama Kuu ya |
Pretoria, anatoa hotuba kali kabla hajafungwa kwa muda wa miaka 25 katika gereza lililo kisiwani Robben. | |
1960–1961 | Zaire (koloni la zamani la Ubelgiji) linapata uhuru kutoka kwa Wabelgiji mwaka 1960. Halafu katika mji wa Elisabethville( sasa Lubumbashi ), kiongozi mzalendo Patrice Lumumba aliuwawa mwaka 1961, na kanali Joseph Desere Mobuto (30) ambaye alikuja kuwa raisi. (Bill Berkeley, ‘Zaire: An African Horror Story’, The Atlantic Monthly, August 1993; rpt. Atlantic Online) |
1962 | Algeria inapata uhuru kutoka kwa Wafaransa, zaidi ya walowezi 900,000 wanaihama nchi mpya. |
1963 | Kenya inatangaza uhuru kutoka kwa Waingereza |
1963 | Mkataba wa umoja wa nchi huru za Afrika, 25 Mei 1963 |
Mid-60s | Nchi nyingi za Afrika zinapata uhuru na kipindi cha ukoloni kinaisha. Vile vile utawala wa uchumi na utamaduni wa magharibi na uchu wa mali na madaraka vinaongeza matatizo yanayozikumba nchi huru za Kiafrika. |
1965 | Rodesia: kutangazwa kwa utawala wa watu wachache |
1966 | Bechuanaland inapata uhuru na kuwa Botswana |
1970s | Wareno wanapoteza makoloni ya Afrika, pamoja na Angola na Msumbiji |
1976 | Cheikh Anta Diop( Senegal , 1923-1986), moja wa |
wanataaluma wa Afrika wa karne ya 20, anatoa kitabu, Afrika chanzo cha Ustaarabu kuondoa uvumi (kuhusu historia ya Afrika) tulio jifunza na kusahihisha kwa kizazi kijacho. | |
1980 | Zimbabwe ( zamani Rodesia ya Kusini inapata uhuru kutoka kwa walowezi wa kizungu baada ya miaka kadhaa ya uadui |
1970s–1980s | Watawala wachache wa Kizungu Afrika Kusini wanasisitiza kuendeleza ubaguzi na mfumo usio na usawa wa ubaguzi wa rangi kupelekea vurugu, uadui, migomo na mauaji kutawala. |
1986 | Mnigeria mwandishi wa tamthilia za fasihi Wole Soyinka anatuzwa zawadi ya Nobel 1986. |
1988 | Mmisri mwandishi wa hadithi na hadithi fupi Nahfouz anatuzwa zawadi ya Nobel 1988, mwandishi wa kwanza kushinda akiwa Kiarabu ndiyo lugha yake ya asili(ya kwanza) |
1994 1996 | Wahutu waliua Watusi wapatao 1,000,000, huku wakiogopa serikali ya Kitusi kulipa kisasi zaidi ya wahutu millioni 1 walihama Rwanda kwa mkupuo na kuvuta hisia dunia nzima. Wakimizi wa Kihutu kama 500,000 walirudi Rwanda kutoka Zaire kuepuka vita nchini zaire |
2001 | Baada ya miaka 38 ya uwepo,OAU (http:// oau.oua.org) inageuzwa kuwa Umoja wa Afrika (AU) |
Kalenda-Nchi za Afrika katika mpangilio wao wa kupata uhuru
Imenukuliwa kutoka: Decolonization of Africa, Wikipedia, Website
Nyenzo 2: Jedwali la Kalenda ya matukio ya Kiafrika