Sehemu ya 5: Kutumia kazi za sanaa kujifunza mambo ya kale

Swali Lengwa muhimu: unawezaje kutumia kazi za sanaa na ushahidi mwingine kutafita historia ya mahali fulani na ya kitaifa?

Maneno muhimu: kazi za sanaa; ushahidi; kazi za makundi; historia ya mahali; mazingira; kuuliza

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia kazi za sanaa kusaidia wanafunzi kuibua maswali juu ya mambo ya kale na kuifahamu historia yao;
  • umeandaa vipindi vinavyowafanya wanafunzi kujitambua wao kwa kufikiri na kujihusianisha na historia ya taifa lao;
  • Umetumia wataalamu wa ndani na mazingira ya mahali hapo katika kipindi chako kuamsha hamasa ya wanafunzi ya kutaka kujua historia yao.

Utangulizi

Kujifahamu wewe ni nani na kujitambua kunaimarishwa kama una uelewa mpana juu ya utambulisho wako na unaweza kuona nafasi yako katika maisha kwa ujumla. Kujifunza kilichotokea zamani kunaweza kuchangia hili. Kupitia kazi za sehemu hii,utawahamasisha wanafunzi wako kufikiria jinsi walivyosehemu ya historia hiyo. Kwa kutumia kazi za makundi, kualika wageni darasani na kazi za mikono, kuchunguza kazi za sanaa kutawafanya wanafunzi kushirikishana mawazo na kukuza ujuzi wao katika historia.

Nyenzo-rejea ya 3: Matukio muhimu kuelekea uhuru