Somo la 1
Kutumia kazi za sanaa au kuangalia picha zao ni njia yakuwafanya wawe wasikivu kwa dhana halisi ya historia na tafsiri yake. Kitu kinachoweza kukusaidia katika kazi hii ni kukusanya nyenzo kama zilivyo na kadili unavyoweza. Daima inawezekana kutafuta vyombo vya zamani na kazi za sanaa kutoka nyumbani na sokoni.
Sehemu hii itakusaidia kupanga shughuli kwa wanafunzi wako kufikiri jinsi vitu tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku vilivyobadilika. Kwa mfano, vitu tunavyotumia kupikia sasa na tulivyotumia zamani tunaweza kupata picha namna gani watu waliishi. Tunaweza kulinganisha vyombo na kutokana na ulinganisho huo, kubuni juu ya maisha yalivyokuwa zamani kwa kutumia kazi za sanaa kama hizo. Hili litawahamasisha wanafunzi kujitafakari nafasi yao katika jamii yao na historia yake.
Uchunguzi kifani ya 1: Uchunguzi wa vitu
Bwana Ndomba, mwalimu wa darasa la 5 mjini Mbinga, Tanzania ameamua kutumia kazi za sanaa zilizotumika kwa kilimo katika somo lake kuamusha udadisi wa wanafunzi na kuwahamasisha kufikiri kihistoria.
Hupanga darasa katika makundi, na kuwapa kila kundi kazi halisi za sanaa au picha mojawapo. Huwataka kuangalia picha au vitu kwa undani na kuandika kadili wanavyoweza juu ya vitu au picha hizo. Wanafunzi wake hufanya vizuri,kwa kuwa hupenda majadiliano, na inaeleweka kwa Ndomba kuwa wanavutiwa na wanafurahia kudadisi juu ya kazi za sanaa.( rejea Nyenzo muhimu: utumiaji wa kazi za makundi darasani )
Baada ya dakika chache, hulitaka kila kundi kubadilishana picha au kazi za sanaa zao na kundi jingine na kufanya tena zoezi lile. Wanapo maliza huamuru makundi mawili kuungana na kushirikishana mawazo yao juu ya picha na kazi za sanaa. Wanafikiri nini juu ya kazi hizo za sanaa?
Zimetengenezwa kwa kutumia nini? Zimetengenezwaje? Wanakubaliana kuandika dondoo tano kwa kila kazi ya sanaa, na kila kundi hushughulika na picha au kazi moja ya sanaa.
Bwana Ndomba huweka kazi za sanaa mezani na dondoo zake tano na kuweka mahali wazi kwa siku kadhaa ili wote waone.
Mwishoni mwa juma, hutaka kila kundi kuandika kwenye upande mmoja wa karatasi juu ya kile walicho na uhakika nacho, na kwa upande mwingine wa karatasi waandike vitu ambavyo hawana uhakika navyo pamoja na maswali yoyote wanayoweza kuwa nayo. Kwake, sio muhimu wakubaliane juu ya kitu, lakini anataka majadiliano yaliyochangamka juu ya yanayodhaniwa kuwa ni matumizi yake na umri wa kitu hicho.
Shughuli ya 1: Kuwa mtaalamu wa historia wa kutumia kazi za sanaa.
Rejea nyenzo 1 : kutumia kazi za sanaa darasani kabla ya kuanza kipindi.
Waamuru wanafunzi kuleta vitu vyovyote vya kitamaduni walivyonavyo majumbani. Waambie unataka kitu kilicho cha zamani kadili inavyo wezekana, labda kilichotumiwa na babu zao au nyuma yao. Lakini wasisitize kuvitunza kwa uangalifu visiharibiwe. Kuwe na meza tayari kwa kuviweka pindi wanafunzi watakapoleta siku ya pili.
Waeleze wanafunzi wako kuwa watakuwa wataalamu wa kuunganisha pamoja ushahidi na taarifa nyingi iwezekanavyo kuhusu vitu vyao.
Watake katika jozi waangalie kazi za sanaa zote na kuziita majina na kuorodhesha katika daftari zao. Kwa kuangalia na kushika, watake kuandika wanachofikiri kimetumika kuzitengeneza, jinsi kilivyotengenezwa na matumizi yake. Unaweza kuwapa karatasi kwa matumizi hayo.
Angalia kazi za sanaa kama darasa kwa zamu na jadili mawazo juu ya sanaa hizo. Kubaliana na wazo lililotolewa na wengi na mtake aliyeleta hicho kitu aeleze anajua nini juu yake. Au wapeleke nyumbani na baadhi ya maswali ya kuuliza na kuleta majibu kwa lengo la kushirikishana na wengine siku inayofuata.
Sehemu ya 5: Kutumia kazi za sanaa kujifunza mambo ya kale