Somo la 2
Moja ya malengo ya kufundisha historia kwa wanafunzi wako ni kuwawezesha kujielewa na kujigundua na kuelewa utambulisho wa jamii zao. Kama mwalimu wa mafunzo ya jamii, hata kama wa shule za msingi unatakiwa kutafuta njia zinazovutia za kuwasaidia wanafunzi kujua ya kale na historia yao. Kwa kuzingatia namna utamaduni wao, shughuli za kila siku na vitu vitumikavyo vilivyobadilika husaidia kujenga utambulisho huu.
Uchunguzi kifani ya 2: Mafunzo ya mavazi ya asili
Bibi Ndonga amewaalika wazee wawili kutoka katika jamii kuja darasani wakiwa na mavazi yao ya asili na kuzungumza kuhusu nini kimebadilika kwenye mavazi ya asili tangu utoto wao.
Kabla ya ziara, Bibi Ndonga husoma Nyenzo muhimu: matumizi ya jamii/mazingira ya mahali kama nyenzo muhimu; na pamoja na wanafunzi wake, huandaa ziara hiyo. Mara wakikubaliana kuhusu muda na tarehe, wanafunzi huandaa maswali ya kuwauliza wageni juu ya kile kilichobadilika kulingana na wakati.
Siku ya ziara, darasa linapangwa na baadhi kwenda kuwakaribisha wageni. Darasa limesisimuka lakini lina aibuaibu kwa wageni. Hata hivyo, wageni wamefurahishwa kuja na kuongea. Pia na kwamba kila mmoja alitulia na kukawa na mjadala mzito juu ya mavazi waliyovaa na umuhimu wa kila kipande cha nguo hizo. Pia wageni walileta baadhi ya mavazi ya asili waliyotumia wazazi wao ili watoto wayaone.
Baada ya wageni kuondoka, Bibi Ndonga anawauliza wanafunzi kuhusu kitu kipya walichojifunza na anashangazwa na kuridhishwa kwa namna wanavyo kumbuka na kulipenda tukio hilo.
Shughuli ya 2: Uchunguzi wa utaalam/ujuzi wa asili
Shughuli hii inalenga kuweka mwongozo, kama mwalimu, unaweza kutumia kufanyia mjadala darasani kuhusu dhana yoyote ya mafunzo ya jamii au historia. Kwa maana hiyo, tunaangalia kazi za sanaa na matumizi yake ya asili.
Waandalie wanafunzi wako ziara ya kumtembelea fundi asilia au waalike shule kuongea na wanafunzi kuhusu ufundi wao wa sasa na namna ulivyokuwa siku za nyuma.
Kabla ya ziara utahitaji kupanga tarehe na muda na nini unataka kuongelea, ili wageni wajiandae nini cha kuleta.
Halafu, pamoja na wanafunzi wako amua ni vitu gani wanataka kuvijua na maswali gani wanataka kuuliza kuhusu kazi za sanaa ambazo wageni wanaweza kuwaonyesha au kuviona wakati wa ziara yao. Inawezekana wageni wakafanya maonesho mbele ya darasa.
Siku ya ziara, waambie wanafunzi wafurahie ziara na kuwaheshimu wakubwa.
Katika kipindi kinachofuata, jadili matokeo ya utafiti na watake wanafunzi katika makundi ya watu wanne kuchagua kitu kimoja kukichora na kuandika wanachokiweza kuhusiana nacho kutokana na kumbukumbu na dondoo walizochukua.(rejea nyenzo muhimu : Matumizi ya kazi za makundi darasani.)
Watake wanafunzi kuweka kazi zao ukutani ili wote wazione na kusoma
Unaweza kuandaa kipindi cha ufundi pamoja na wageni ili wanafunzi waweze kufanya kwa vitendo.
Somo la 1