Nyenzo-rejea ya 1: Matumizi ya kazi za sanaa darasani

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Nafasi ya kushika kazi halisi za sanaa ni uzoefu pekee. Kwa sababu ambazo hakuna mwenye uhakika nazo, kitendo cha kushika kitu ambacho dhahiri kina historia na hadithi yake, huhamasisha kila mmoja. Bila shaka wanafunzi watakuwa wadadisi juu ya kazi za sanaa na hii itapelekea kuwa na mjadala mzuri.

Kushika kazi ya sanaa huwafanya wanafunzi kutumia hisia zao kukuza udadisi na ujuzi wa kutatua matatizo, kuimarisha uelewa wao wa wakati ule na kuwajali watu wa kale.

Nini lengo la kipindi cha kazi za sanaa?

Vipindi vya kazi za sanaa vinaweza kutumika kwa:

  • kuwapa motisha wanafunzi mwanzoni mwa mada;
  • kuwavutia na kuvuta usikivu wa wanafunzi
  • kupanua ufahamu wao juu ya mada wanayojifunza
  • kuwapelekea kujifunza kiundani na kwa mapana zaidi
  • Kusimama kama daraja kati ya baadhi ya masomo tofauti na vitu vinavyozungumziwa
  • Kupembua ukuaji wa ufahamu wa wanafunzi mwishoni mwa kipindi. Maswali gani niulize wakati wa kipindi cha kazi za sanaa?

Aina ya maswali unayouliza yatategemea ni kazi gani ya sanaa unatumia. Maswali ya hapa chini yatakusaidia kupata majibu ya kazi za sanaa.

Maswali kuhusu tabia za wazi za kitu

  • Inaonekanaje? Hisia, harufu na sauti yake?
  • Ni kikubwa kiasi gani?
  • Kina umbo gani?
  • kina rangi gani?
  • Kina uzito gani?
  • Je kina alama yoyote inayotuonyesha namna kilivyotengenezwa, kilivyo tumiwa au kutunzwa?
  • Kimetengenezwa kwa kutumia nini?
  • Ni cha kawaida au chakipekee?
  • Ni kizima au sehemu ya kitu chote?
  • Je kipo katika hali nzuri au kimechakaa?
  • Je, kimebadilishwa kimeigwa, kimerekebishwa au kimegeuzwa?

Maswali kuhusu ubunifu na matengenezo ya kitu

  • Kimetengenezwa kwa vifaa gani?
  • Kwanini vifaa hivyo vilichaguliwa?
  • Je vifaa tofauti vingetumika?
  • Kinavutia kukiangalia?
  • Kinaweza kuwa kilitengenezwa lini na wapi?
  • kilitengenezwa kwa mkono au kwa mashine?
  • Nani anaweza kuwa alitengeneza?
  • Kimetengenezwa katika kipande kimoja au vipande tofauti?
  • Kinaweza kuvunjwa vipande vipande?
  • Kimeunganishwaje?
  • Kinawezaje kufanya kazi?
  • Kimerembwa au kawaida?
  • Kuna alama zozote/taswira kwenye kitu?
  • Hivi vinatuambia nini kuhusu watu waliokitengeneza au wanaokimiliki na wakati tunapojifunza?

Maswali kuhusu umuhimu na thamani ya kitu 

  • Kifaa hicho kilileta utofauti gani katika maisha ya watu?
  • Kilikuwa na umuhimu gani: watu waliokitengeneza au waliokimiliki; watu wa leo?
  • Kinatuambia nini kuhusu watu waliokimiliki?
  • Kimetengenezwa kwa wingi, mara chache au kwa upekee?
  • Ni muhimu kiuchumi/kihistoria/kiutamaduni?
  • Ni kwa namna gani ni muhimu leo?

Maswali kuhusu kazi ya kifaa

  • Ni nini?
  • Kwa nini kilitengenezwa?
  • Jinsi gani kinaweza kuwa kilitengenezwa?
  • Nani anadhaniwa kukitumia?
  • Ujuzi gani ulihitajika kukitumia?
  • Kingeweza kutumiwaje?
  • Wapi kinadhaniwa kutumiwa?
  • Je kinadhaniwa kutumiwa na vitu vingine?
  • Matumizi yake yamebadilika?

Kufundisha kwa kutumia vitu-baadhi ya mbinu

Baadhi ya mbinu zilizoelezewa hapo chini zinaweza kutumiwa na wanafunzi wakati wa kusoma nyaraka, machapisho na rangi. kichokoo kinachoonekana

Vitu vinaweza kutumika kuanzisha majadiliano mwanzoni mwa kipindi. Vitu hivyohivyo vinaweza kutumika kurejea walichojifunza wanafunzi na kuona kama moja ya mawazo na ufahamu wao umebadilika kutokana na kipindi hicho.

utafiti wa kihistoria

Uchaguzi wa vitu unaweza kutumika na wanafunzi kwa mazoezi ya utafiti kihistoria-kupata taarifa kutoka vyanzo. Wape muda wanafunzi kuona vitu kwa umakini kabla ya kutafiti baadhi ya maswali yafuatayo:

  • Kimetengenezwa kwa kutumia nini?
  • Vifaa au mbinu gani zilihitajika kukitengeneza?
  • Nani anadhaniwa kukitengeneza?
  • Je kulihitajika ujuzi wa kipekee kukitengeneza?
  • Kimerembwa? Namna gani?
  • Nani anadhaniwa kukitumia?
  • Kilikuwa ni kwa matumizi gani?
  • Je kilifanya kazi au kilitumika kwa njia nyingine?
  • Kinauzito au ukubwa kiasi gani?
  • Ni cha muhimu au kitu adimu? 

Kulinganisha na kuvihusianisha vitu

Tumia vitu viwili au taswira kwa pamoja na watake wanafunzi kulinganisha, kutafiti ufanano na utofauti kati ya vitu na taswira. Tumia makundi ya vitu na ongelea uhusiano kati yao.

Uwakilishi na ufasiri

Baadhi ya kazi ya sanaa zinaweza kuonyesha ushahidi wa mtazamo fulani. Nani alitengeneza kitu hicho na kwa malengo gani? Ni kitu halisi au propaganda tu? Kinatupa habari yote? Kinatuambia nini?

Shughuli nyingine zitumiazo vitu ni

Shughuli za utabiri-waonyeshe wanafunzi kifaa na watake kufikiria kipindi gani cha kihistoria kinahusiana na kifaa hicho.

Uchunguzi kifani-wanafunzi wanaweza kutumia kitu kimoja au vingi kujenga uchunguzi kifani, kwa mfano maisha ya Afrika Mashariki kabla ya kuja Waarabu.

Makundi-wanafunzi wanaweza kukusanya vitu katika jozi zinazokuwa na vitu fulani vinavyofanana (kama vifaa fulani, nchi vinakotoka, namna vilivyotumika). Wanafunzi wanaweza kufikiria namna ya kutengeneza makumbusho kwa kuweka vitu katika makundi na kwa namna tofauti.

Uandishi wa kichwa cha habari-wanafunzi wanaweza kuandika vichwa vyao vya habari au alama za maonyesho, au kutoka mtazamo wa kisasa au kama walikuwa wanandika kwa muda huohuo wakati kitu kinatengenezwa.

Hisia zenye ufahamu-wanafunzi wanaweza kuorodhesha sifa zinazoelezea namna wanavyojisikia kuhusu kitu, wakionyesha ufahamu na kuguswa juu ya vitu husika.

Majibu ya ubunifu-wanafunzi wanaweza kuitikia vitu kupitia ubunifu, tamthilia au sanaa za maonyesho.

Ni masomo gani yanaweza kusaidiwa na matumizi ya kazi za sanaa?

kujifunza kutokana na vitu ni msaada kwa somo katika mitaala mbalimbali

  • Historia: ufahamu wa mtiririko, hisia na ujuzi wa msingi
  • Sayansi: tabia za vitu, uchunguzi, kulinganisha, mchanganuo, na ujuzi wa kudadisi.
  • Kingereza: kuuliza na kujibu maswali, nyenzo za muktadha.
  • Tamthilia: nyenzo chokoo, kujenga hisia
  • Sanaa na ubunifu: nyenzo chokoo, nyenzo za muktadha

Nyenzo-rejea ya 2: Sanaa zangu