Somo la 2

Vinyago vya jadi vya Kiafrika vilifikiriwa kuwa ni vitu vya muhimu sana kwa sababu vilifanya kazi muhimu ya mizimu katika imani za Kiafrika. Kusudi la kwanza la kutengeneza vinyago vya Kiafrika lilikuwa ni kwa ajili ya sherehe maalumu au shughuli muhimu za kijamii. Si kama Ulaya Magharibi amabako vinyago vilichukuliwa kama njia ya “kuuwakisha” mzimu, vinyago vya Kiafrika vilieleweka kuwa pale ambako mzimu “uliumbwa”.

Kwa maneno mengine, pale ambapo mtu anavaa kinyago, pamoja na vazi ambalo limefunika kuanzia kichwani hadi miguuni, mtu huyo kwa kweli “anakuwa” ni mfano wa mzimu amabao umekusudiwa kuwakilishwa, ukipewa uhai kwa kupitia ishara, sauti, shughuli mbalimbali na hata hali yao ya kupagawa.

Katika Uchunguzi kifani 2 , mwalimu hutumia kazi za vikundi kuwawezesha wanafunzi wake kufikiri na kuwaruhusu kubadilishana mawazo juu ya madhumuni ya vinyago tofauti. Katika shughuli 2, wanafunzi wako watatengeneza vinyago vyao wenyewe, wakiwa wametafakari maswali kama yale yaliyoulizwa kwenye uchunguzi kifani.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuchunguza alama na maana kwenye vinyago vya jadi vya Kiafrika

Bi. Sungi ni mwalimu wa sanaa katika shule ya Ihanja, mkoa wa Singida. Ameamua kufanya uchunguzi wa vinyago vya jadi vya Kiafrika akiwa na mitazamo mitatu akilini mwake:

Kuangalia juu ya uzoefu na matumizi ya kazi za sanaa Afrika nzima. Kuchunguza jinsi alama zilizo kwenye kazi ya sanaa zinavyopeleka maana halisi katika mtazamo wa kiutamaduni.

Kuwasaidia wanafunzi wake kutengeneza vinyago vyao wenyewe. Anapanga kutumia kama vipindi viwili vinavyofuatana vya somo la sanaa ili kufikia malengo yake.

Bi. Sungi anaanza kwa kuwaonyesha wanafunzi wake vitabu vya picha na majarida yaliyo na picha za vinyago vya jadi kutoka eneo lote la Afrika, kusini mwa jangwa la sahara. (Angalia Nyenzo rejea muhimu 3: Kinyago cha Afrika kwa mfano.)

Analiambia darasa, likiwa katika makundi, kuchunguza baadhi ya vitabu kwa pamoja na kupata matumizi ya kawaida ya vinyago katika maisha ya kijamii kwenye mazingira tofauti ya kiutamaduni. Kila kundi linaandaa orodha ya matambiko na kazi za kiutamaduni za vinyago vya Kiafrika.

Kwa kutumia Nyenzo rejea muhimu 4: Andalio la somo la vinyago vya Afrika ya Mashariki , Bi. Sungi anaendelea kuonyesha vinyago maalumu kutoka Afrika Mashariki, ambavyo ni vya mitindo mingi sana ikiendana na matambiko na ishara ya uwezo. Anakazia kwenye alama muhimu za vinyago. Baadaye anawapa wanafunzi wake muda wa kutengeneza vinyago vyao wenyewe.

Shughuli ya 2: Kutengeneza vinyago vinavyowakilisha hisia na ujumbe wa jamii

Kabla ya somo, kusanya pamoja vitabu vya picha na majarida yenye vinyago vya Kiafrika kutoka sehemu mbalimbali na, ikiwezekana, baadhi ya mifano ya vinyago halisi vya mahali hapo.

Waambie wanafunzi waziangalie nyenzo rejea muhimu ulizozikusanya kupata mwelekeo wa vinyago vyao wenyewe.

Wanavyopangilia vinyago vyao, wanafunzi wanahitaji kufikiria ni ujumbe gani wanataka vinyago vyao vibebe. Wakumbushe kuwa wanatakiwa kufikiria juu ya:

Alama za usoni; alama wanazoweza kutumia; jinsi ya kuteka hisia; rangi.

Waambie wapangilie vinyago vyao katika vipande vidogo vya karatasi/kadi kwanza, kabla ya kutengeneza picha kubwa au mfano wa vinyago kutokana na kadi hizo hizo.

Itabidi uwape vipindi vya sanaa kadhaa kwa ajili ya kazi hii. Onyesha vinyago vyilivyokamilika ili wote waone na alika madarasa mengine yaje yaone.