Somo la 3

Kutengeneza ughushi wao wenyewe ni muhimu kwa wanafunzi wako na watataka kushirikisha mafanikio yao kwa watu wengine. Katika sehemu hii, tunashauri kuwe na maonyesho shuleni ya ughushi na vitu vingine ambavyo vimetengenezwa na wanafunzi kama njia ya kuendeleza na kuhifadhi fahari ya wanafunzi wako katika urithi wao wa utamaduni. Ughushi kutoka kwenye jamii ya hapo ambao hauwezi kubebeka au haupatikani unaweza kuonyeshwa kwa kutumia picha zilizokatwa kutoka magazetini na vyanzo vingine.

Uchunguzi kifani 3 unaonyesha jinsi darasa moja, likifanya kazi kwa makundi, lilivyojihusisha kwenye hatua zote za maonyesho, kutoka

kwenye kuyaandaa hadi kuongea na wageni. Kwenye Shughuli muhimu , wanafunzi wako wataandaa onyesho ambalo wageni watatembelea bila wenyeji, hivyo kazi ya kuweka alama zinazojieleza na za kuvutia ni muhimu sana.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuonyesha ughushi shuleni siku isiyo ya masomo

Siku ambazo si za masomo za shule ya msingi ya Ilemela kwa kawaida hufanyika kuelekea mwishoni mwa mwaka wa shule. Bwana Koku, amabaye ni mwalimu wa sanaa wa wanafunzi wa drasa la nne, aliiambia kamati ya maandalizi ya siku hiyo kuweka sehemu kwenye chumba cha maonyesho ili darasa lake lionyeshe ughushi waliotengeneza darasani au waliokusanya kutoka vyanzo mbalimbali katika jamii. Ombi lake lilikubalika.

Katika kipindi cha maandalizi, Bwana Koku aliliongoza darasa lake kuandaa maonyesho. Aliwagawa wanafunzi katika makundi manne. Kundi la kwanza lilitakiwa kukusanya na kuweka utambulisho kwenye michoro yote, picha na vitu ambavyo vilitambulika kama vifaa vya nyumbani. Kundi la pili lilipewa kazi kwa upande wa vifaa vya muziki, kundi la tatu lilipewa kazi kwenye sehemu ya usonara na kundi la nne lilipewa upande wa uchongaji.

Shughuli zote hizo zilichukua vipindi viwili. Katika kipindi cha tatu, kulikuwa na kuelezea makusanyo hayo darasani kama ambavyo mtu angeweza kuelezea kwa wageni. Siku ilipowadia, darasa lilionyesha vitu vikiwa vimepangwa katika makundi manne, na wanafunzi wanne wakitoa maelezo kwa wazazi na wanajamii wengine waliotembelea meza ya maonyesho ya darasa.

Mwisho wa siku, meza ya ughushi ilizawadiwa kikombe cha kuwa meza bora kwenye chumba cha maonyesho.

Shughuli muhimu: Kuandaa maonyesho ya ughushi

Waambie wanafunzi wako walete darasani michoro, ughushi, vinyago, vyungu na vikapu iwe kutoka nyumbani au walivyotengeneza wakati wa vipindi vya sanaa.

Andaa kadi tano. Kwa kila kadi, andika moja ya maneno yafuatayo: wachoraji, wachongaji, wafinyanzi, mafundi seremala, wasusi. Ligawe darasa lako katika makundi matano na toa kadi moja kwa kila kundi.

Waambie kila kundi wachague vitu walivyoleta vinavyoendana na majina ya kadi zao na waviweke sehemu tofauti.

Baada ya hapo, yaambie makundi yalinganishe vitu. Majadiliano yatakayoendelea hapa ni muhimu kujenga uwezo wa wanafunzi wa kutofautisha na uwezo wa kufikiri; na pia yatasaidia kutambua mambo ya msingi wanayotaka kuyajumuisha kwenye utambulisho wa vitu.

Waambie kila kundi liandike jina na utambulisho wenye maelezo kwa kila kitu kwenye kundi lao.

Waambie kila kundi, wapange vitu vyao kwa ajili ya watu kuangalia, wakati wanafunzi wengine wakijifanya kuwa ni wageni. Waambie “wageni” watoe maoni yao ni jinsi gani makundi yangeweza kuboresha utambulisho wao.

Andaa labels za mwisho na lipe darasa lako muda wa kuandaa maonyesho.

Andaa orodha ya wanafunzi watakaojifanya wamekuja kutembelea maonyesho. Hii inaweza kufanyika muda wa mapumziko au muda wa chakula cha mchana tu.

Baada ya maonyesho,jadili na wanafunzi wako juu ya walichopata kutokana na uzoefu kwa misingi ya uelewa wa ughushi na kujihusisha kwao kwenye tukio kama hilo.

Nyenzo-rejea ya 1: Kazi ya nyumbani ya kuorodhesha kazi za ughushi za mahali hapo