Nyenzo-rejea ya 4: Andalio la somo kuhusu vinyago vya Afrika ya Mashariki

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Chanzo halisi: Masks of the World, Website

Kwa jumla kuna aina tatu za vinyago; vya usoni, vya kichwani (ambavyo kama jina linavyooyesha vinavaliwa kichwani), na vya mwilini, ambavyo hufunika sehemu kubwa ya mwili wa mchezaji na vinategemewa kubadili mwonekano wake kutoka kwa watu wanaomfahamu. Vinyago vya mwilini wakati mwingine hufunika mwili tu na huvaliwa pamoja na vya usoni au vya kichwani.

Vinyago vyote huwakilisha mizimu au wazee waliokufa,na vilikuwa vikitumika sana kwenye sherehe za jando kama muonesho wa mwendelezo, hofu na uadilifu. Vilevile vilitumika kwenye ngoma na matukio ya sikukuu, kwa mfano sharehe za mavuno.

Vinyago vya kichwani (mapiko; umoja lipiko) vinafahamika sana kwa mfanano wake. Vingi vina nywele halisi za mwanadamu zilizonyolewa vizuri, nyuso nzuri na midomo ya wazi isiyokuwa na meno, masikio makubwa au vizibo vya mdomo. Vinatumika katika mchezo wa mapiko na michezo mingine. Japo kuwa vichwa vya wanaume na wanawake wote vinaweza kutumika, ni mara chache sana kuona vichwa vya wanawake. Mchezaji hupumua na kuona kupitia tundu dogo lililoko mdomoni.

Mapiko si jina linapewa kwa vinyago (kwa kawaida vya kichwani) tu, bali pia ni jina la ngoma, jina la nguvu inayotisha, na vilevile ni jina la moja kati ya hatua za unyago wa wanaume, wakati mhusika anapoingizwa kwenye siri za Mapiko. Vinyago vyenyewe vimetengenezwa katika sehemu ya siri porini inayojulikana kama Mpolo, ambayo wanawake wanakatazwa kupafikia. Pale vinapokuwa havitumiki, vinyago huwekwa

Mpolo, na kijadi vilichomwa moto vilipovunjika au kubadilishwa na vingine vipya.

Matokeo

Wanafunzi watajenga tathmini mbalimbali za vinyago na watatengeneza vinyago;+

Vifaa

karatasi ya kuchorea

kadi

penseli

udongo

karatasi katika rangi anuwai

kalamu za rangi

rangi ya bango

shanga, magamba n.k

mkasi

gundi

1.     Kusanya baadhi ya picha za vinyago za kuwaonyesha wanafunzi wako.

2.     Jadili taswira za vinyago na uashiria wake.

3.     Waambie wanafunzi watengeneze mchoro wa mwanzo wa kinyago.

4.     Wafuatishie michoro kwenye kadi halafu wachore vinyago vyao. Waambie wanafunzi kuwa wanaweza kubadili baadhi ya vitu kwenye nyuso za vinyago vyao. Mfuatisho ni mwongozo tu wa mahali pa kuweka macho na mdomo endapo wangependa kuvivaa vinyago vyao.

5.     Paka vinyago rangi na viache vikauke.

6.     Toa vinyago na andaa vitu ambavyo vitaambatana navyo kama nywele na mkanda wa kukishikilia kichwani.

7.     Wape wanafunzi muda wa kupamba vinyago vyao.

Nyenzo-rejea ya 3: Kinyago cha kiafrika

Sehemu ya 2: Kuandaa Shughuli za Sanaa kwa Vitendo