Sehemu ya 2: Kuandaa Shughuli za Sanaa kwa Vitendo

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kuuliza maswali kuhusu na kutengeneza sanaa ya mahali hapo?

Maneno muhimu: ustadi; utafiti; mawasilisho; vitendo; utamaduni

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umepata ni nini wanafunzi tayari wanajua juu ya ufundi wa mahali hapo;
  • Umewapanga wanafunzi wako katika makundi madogo kufanya shughuli za kiutafiti;
  • Umeandaa shughuli za vitendo ili kuwasaidia wanafunzi watengeneze na kutathimini vifaa vyao vya ufundi.

Utangulizi

Wanafunzi wengi tayari watakuwa na uelewa juu ya ufundi wa mahali hapo na baadhi yao wanaweza wakawa na ujuzi mkubwa wa kutengeneza baadhi ya hivyo vifaa. Wigo wa ufundi mahali hapo unaweza kujumuisha vitu kama utungaji shanga, ufinyanzi, uchongaji, uchoraji na uhunzi.

Ni muhimu kutambua wanafunzi wanachokifahamu kwanza, na kutumia huo ufahamu kama msingi wa kupangilia shughuli kuzunguka ufundi wa mahali hapo. Katika sehemu hii, utawahimiza wanafunzi kuchangia mawazo na kujenga uelewa wao juu ya thamani na matumizi ya huu ufundi wa jadi. Njia mojawapo muhimu ni kuwaruhusu wanafunzi kutengeneze zana zao wenyewe; hii hutoa nafasi kwao kupangilia na kutathimini kazi zao.

Nyenzo-rejea ya 4: Andalio la somo kuhusu vinyago vya Afrika ya Mashariki