Somo la 3

Unapojifunza mada ya vitendo kama kazi za ufundi, ni muhimu wanafunzi wako wakapata nafasi ya kutumia vifaa vya kujitengenezea wenyewe au walau waone mtu akivitumia kutengeneza vitu vya ufundi.

Uchunguzi kifani 3 unaonyesha jinsi mwalimu mmoja alivyokusanya udongo wa mfinyanzi kutoka pembeni mwa mto ili wanafunzi wake waweze kutengeneza vyungu vya udongo wao wenyewe. Kwa kuwapa vifaa na kuangalia nini wanachoweza kufanya, wanafunzi wanapata mwanga mzuri wa ujuzi wanaohitaji. Kama una uhakika wa upatikanaji wa vifaa,

waandalie wanafunzi wako watengeneze stadi zao wenyewe.Hizi zinaweza baadae kuonyeshwa kwa wanafunzi wengine au kwa wazazi. Kwa wanafunzi wakubwa, wahimize wathamanishe kazi zao-nini walichohisi kimeenda vizuri? Nini wangeweza kuboresha hapo baadae?

Shughuli muhimu inaelezea jinsi ya kuandaa maonyesho ya ufundi. Hii ni njia nyingine ya kuwahamasisha wanafunzi na kuwawezesha kuelewa vizuri uwezo wa ufundi wa mahali hapo.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutengeneza vyungu

Bi. Kapunga alikuwa anafundisha somo juu ya vyungu vya asili. Alianza kwa kuwataka wanafunzi watoe uzoefu wao juu ya vyungu vya asili na vifaa vingine. Wanafunzi walikuwa na uelewa mzuri juu ya matumizi ya vifaa hivyo wakati wa mavuno na wakati wa sherehe za ndoa na za kidini. Wanafunzi vilevile waliongelea juu ya vyungu tofauti wanavyovifahamu, kama vile vya kuhifadhia mapambo. Wakati wanaongea hayo, Bi. Kapunga alitengeneza orodha ya vyungu vya asili ubaoni.

Bi. Kapunga alikuwa ameleta baadhi ya vyungu ambavyo alivipata kwa watu katika jamii anayoishi. Aliwaambia wanafunzi nao wapeleke vyungu walivyokuwa navyo nyumbani ili waweze kuangali maumbo n.k. Baadae, aliwaonyesha jinsi ya kutengeneza chungu kidogo kutokana na udongo aliokuja nao kutoka mtoni. Aliwapa kila kundi la wanafunzi wawili udongo kidogo watengeneze chungu na kukipamba kwa njia yoyote ile waliyoipenda.

Aliwahimiza waangalie mitindo ya asili, na kutoka hapo ndipo wajenge mitazamo yao wenyewe. Vyungu vya wanafunzi viliachwa ili vikauke pembeni mwa darasa ambapo kila mmoja angeweza kuviona. Bi. Kapunga alifurahishwa sana na kazi ya wanafunzi.

Nyenzo rejea muhimu 3: Kutengeneza vyungu inatoa taarifa za msingi.

Shughuli muhimu

Wanafunzi wako wanapokuwa wamemaliza kufanya utafiti juu ya zana waliyoichagua, mualike mtaalamu mmoja wa mahali hapo aje awaonyeshe jinsi zana hizo zinavyotengenezwa, kwa mfano, utungaji shanga au uchongaji, ndipo wanafunzi wanaweza kutambua zaidi ni kwa nini na kwa jinsi gani wanafanya ufundi.

Halafu, waulize wanafunzi wako ni kwa jinsi gani wangependa kuwasilisha utafiti wao na wangependa wafanye hivyo kwa nani. Lipangilie darasa lako katika makundi ambayo yanapendezwa na ufundi wa aina moja au unaofanana ili wajadili mawazo yao.

Jadili baadhi ya mawazo yao.

Kubaliana nao kuhusu tarehe na sehemu kwa ajili ya hili.

Toa muda wa kutosha kwa kila kundi kuandaa kitabu chake, bango, onyesho, uthibitisho wa jinsi ya kutengeneza zana au mawasilisho kwa kutumia mdomo.

Wafanye majaribio ya tukio na waambie kila kundi liwasilishe kazi zake

Siku yenyewe, darasa au shule nyingine, au wazazi wanaalikwa kuja na kuona kazi za wanafunzi. Kila kundi linasimama na kazi zake na kuelezea kwa wageni. Maelezo kwa mdomo yanafuata baada ya kuwa watu wameona zana zilizoonyeshwa.n.k.

Nyenzo-rejea ya 1: Maswali ya utafiti juu ya vifaa vya jadi na kazi zake