Nyenzo-rejea ya 1: Hadithi za ngoma ya Venda

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Hadithi ya ngoma takatifu ya Venda

Hapo zamani za kale, miungu ya mababu iitwayo Mwari iliwapa watu wa Venda ngoma yao takatifu ikiitwa ngoma Lungundu. Katika siku hizi za kale, mababu wa venda waliishi Zimbambwe. Siku moja walipokea ujumbe wa kimungu kwamba wanatakiwa kuchukua ngoma yao takatifu, Ngoma Lugundu, na waelekee kusini.

Ngoma hii ilikuwa kubwa na nzito na ilipaswa kubebwa na wanaume wengi. Ili watunze nguvu za ngoma, ilitakiwa isiguse chini/ardhi.Ikipigwa na mfalme inaweza kusababisha ukungu, mvua ya mawe, mvua, radi au miale ya radi. Kwa muda fulani Mungu mkuu Mwari anaipiga yeye mwenyewe. Wakati huu ngoma ingeonekana kama inajipiga yenyewe. Maadui walikimbia kwa hofu, walizimia au kufa waliposikia midundo yake yenye nguvu.

Nguvu hizi zilisaidia kuwalinda hawa mababu wa Venda wakati wa hii safari na mwishowe walifika wanapoishi leo hii kaskazini mwa Afrika kusini. Hapa kuna ziwa linaloitwa funduzi ambalo ni takatifu kwa wavenda.

Miaka mingi iliyopita, shujaa wa wavenda, aitwaye Thoyo ya Ndou, alipotelea katika ziwa hili akiwa amebeba ngoma hiyo. Watu wengi wanafikiri kuwa haijawahi kuonekana tangia wakati huo, lakini wengine wanaamini kuwa imelindwa na kufichwa katika pango.Thoyo ya Ndou, au mkuu wa Tembo, alikuwa anatamaniwa kwa sababu aliwaunganisha watu wa Venda na kulikuwa na amani na ustawi. Tangu alipopotea, wengi wanasema kuwa kumekuwa na kutoelewana mafarakano/migongano katika familia ya kifalme ya Venda.

Chanzo halisi: Catalogue: Ten Years of Collecting (1979–89), Standard Bank Foundation Collection of African Art, Editors: Hammond-Tooke & Nettleton, 1989

Nyoka/Joka (Chatu)

Katika jimbo la Limpopo kuna ziwa zuri liitwalo Fundulizi.Watu wa Venda wanalichukulia kuwa muhimu sana, eneo lililotakaswa, kwani wanaamini kuwa kuna joka kubwa jeupe linaloishi chini ya Fundudzi. Joka hili ni Mungu wa mtuba. Kwa maneno mangine anahakikisha kuwa watu wana afya nzuri na wana watoto wengi.

Hapo zamani, Mungu huyu aliishi nchi kavu.Alikuwa na ngozi nzuri; na alioa wanawake wanadamu wawili; mmoja mzee na mwingine kijana. Ilitokea kuwa alikuwa akiwatembelea hawa wake zake wawili kila siku usiku sana. Alitembelea vibanda vyao walipokuwa wametingwa na kazi za shamba. Hivyo hawakuwahi kumuona mume wao au kujua alikuwa anafananaje.

Siku moja, mke mdogo aliingiwa na tashwishwi na kuamua kurudi toka shambani mapema na kuchungulia dirishani. Alitishika alipoona kuwa mume wake alikuwa ni joka nene na kupiga kelele. Joka lilikimbia na kuingia ziwani. Tokea hapo kulikuwa na ukame na njaa juu ya ardhi. Wanyama walikufa na hakukuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya mazao.

Hakuna anayejua kilichosababisha balaa hili na wazee walikutana ili kujadiliana juu ya tatizo hilo. Hatimaye, mke mdogo alikiri kuhusika kwa yale yaliyotokea. Walimwomba awasaidie kurudisha rutuba kwenye ardhi. Siku moja alichukua mtungi wenye pombe na kuelekea ziwani. Wanaume walipiga filimbi zao ili kumtia ujasiri. Alitembea kwenye kina kirefu hadi maji yalipofunika kichwa chake, na hakuonekana tena.

Baada ya hili, mvua ilirudi na ukame ukakoma. Mpaka leo, wafalme wa Venda na waganga wa kienyeji/jadi huenda kwenye ziwa Fundudzi na kumwaga pombe majini. Wanaamini kuwa kama pombe itazama, ni dalili za furaha ya Mungu Nyoka na kukubali kwake zawadi yao. Katika mila ya Venda, vijana kuhudhuria shule maalumu ya jando.Hii huwaandaa kwa majukumu yao kama waume na wake ndani ya jamii. Vijana hujifunza ngoma ya domba wanapohudhuria dombani au shule ya jadi. Kabla ya domba haijaanza, kiongozi wa ngoma anaita: ‘Tharu ya mahbidighami!’ (‘Joka linajikunjua’). Wanapocheza ngoma, hutengeneza mstari mrefu kama ‘ nyoka’ kwa kuzunguka moto.

Nyenzo-rejea ya 2: Mila za kienyeji: Mbinu za kuchezangoma katika Tanzania