Nyenzo-rejea ya 1: Kugundua sauti

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Shughuli A: Maswali ya kimuziki kuhusu sauti

Anza kwa kuchunguza sayansi ya sauti na wanafunzi. Gundua haya maswali na wanafunzi wako kwa kutengeneza sauti mbalimbali, katika njia tofauti, kwa kutumia vitu vinavyokuzunguka: dawati, sakafu, kalamu, chupa, ubao au dirisha. Kumbuka, kuongelea juu ya sauti lazima

kuendane na uzoefu tulionao juu ya sauti.

Sauti ni nini?

Nini kitokee ili sisi tusikie sauti? Sauti inasafirije kutufikia sisi?

Nini kinafanya kitu kuwa kifaa cha muziki?

Tunaweza kutumia mwili wetu kama kifaa cha muziki? Kwanini unafikiri kuwa watu wanatumia vifaa vya muziki

kutengeneza muziki? Inatimiza malengo gani?

Unafahamu vifaa gani vya muziki? Unaweza ukaviainisha katika makundi?

Ni kigezo gain ulitumia kuainisha hivyo vifaa?

Shughuli B: Muunganiko wa kisayansi – jinsi gani sauti inasafiri

Umewahi kuona”wimbi la Kimeksiko” (‘Mexcan Wave’) kwenye tukio kubwa la kimichezo? Sauti husafiri kwenye njia sawa na mwendo wa wimbi la Kimeksiko; molekyuli za hewa, kama watu katika mkusanyiko, zinakwenda mbele na kurudi nyuma, zikiungana na kutengeneza wimbi. Molekyuli mojamoja hazisafiri kutoka eneo moja kwenda jingine: molekyuli hutetemeka, kila moja kwenye nafasi yake, isipokuwa

kunapokuwa na kitu kingine karibu na molekyuli zinasogea. Hizi molekyuli zinazotetemeka zinavuta molekyuli nyingine, hivyo basi zinatoka kwenye sehemu zao.

Sauti inaweza kusafiri kwenye hewa kitu chochote kilichotengenezwa kwa molekyuli kama maji, chuma au mti. Sauti husafiri kwa kasi tofauti kutegemeana na kitu inamosafiria.

Shughuli C: Kutengeneza wimbi la sauti

Tengeneza mstari wa wanafunzi kumi waliosimama kwa kufuatana. Upande mmoja, mwambie mwanafunzi mmoja apige chombo cha muziki kama mbiu na mwingine alama kubwa inayosema SAUTI. Upande mwingine, mwabie mwanafunzi abebe picha kubwa ya SIKIO. Wanafunzi wengine kwenye mstari wawe na alama ya HEWA.

Mwambie mwenye mbiu aipige. Mwanafunzi wa kwanza.anayumba mbele na nyuma kwa kutumia mwili wake (huku miguu ikiwa imesimama ardhini); mwanafunzi anayefuata naye anayumba baada ya kuhisi uwepo wa mtetemo wa mwanafunzi wa kwanza, na hivyo hivyo kwa mstari mzima.Mwnafunzi wa mwisho anashikilia alama ya KUSIKIA anapohisi myumbo wa mwanafunzi anayemfuata.

Chanzo halisi: Stomp Online Lessons, Website

Nyenzo-rejea ya 2: Kutengeneza zana