Somo la 1

Hadithi inaweza kusemwa, kuandikwa, kusomwa na kusimuliwa. Inaweza kuwa hadithi ya kweli au ya kutunga. Mara nyingi hadithi zina ujumbe

ndani yake juu ya taratibu za jamii, namna ya kuishi maisha yetu na namna ya kuwajali wangine.

Wewe na wanafunzi wako yawezekana mmeshawahi kuhadithia au kusikia hadithi. Yawezekana pia mmeshaandika baadhi. Sehemu hii itakusaidia kuwajengea wanafunzi wako uelewa wa sanaa ya kuhadithia hadithi na kwamba kuhadithia hadithi kumejikita ndani ya utamaduni wa jamii yenu.

Unaweza kuwa na bahati kwa kumfahamu mtu ndani ya utamaduni wa jamii yenu. Unaweza kuwa na bahati kwa kumfahamu mtu ndani ya jamii yenu mwenye ujuzi wa kuhadithia na ukaweza kuja kuhadithia hadithi darasani kwako (angalia nyenzo rejea muhimu; kutumia jamii/mazingira ya asili kama nyenzo rejea ). Au, katika uchunguzi kifani 1 , unaweza kumtembelea wahadithiaji na kuwarekodi kwenye kanda ili uitumie darasani kwako. Shughuli 1 inapendekeza njia za kuwaandaa wanafunzi kushirikishana hadithi wazipendazo.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia watu wa kawaida kujifunza umuhimu wa kiutamataduni wa hadithi.

Bibi Biyela anafundisha katika Shule ya Msingi Furaha nchini Tanzania. Anajiandaa kwa mada yake unayofuata, ambayo ni ‘Hadithi’. Anapitia vitabu na nyenzo rejea za tovuti juu ya uhadithiaji wa hadithi, uandishi na usomaji. Anajifunza kuwa kuhadithia hadithi kuna umuhimu wa ndani wa kiutamaduni, na anatafuta baadhi ya njia za kufikisha umuhimu huu kwa wanafunzi wake.

Amesikia habari za ajuza/kikongwe mmoja, Bibi Koku, anayeishi jirani ni maarufu kwa uhadidhiaji. Mchana mmoja, anaamua kumtembelea Bibi

Koku na akamuuliza kama atakuwa tayari kuhadithia hadithi wanafunzi wa mwalimu Biyela. wa darasa la nne. Kikongwe huyu anakubali lakini anasema ‘jioni tu’. Anasisitiza kuwa watu wanaohadithia hadithi mchana wanakaribisha njaa katika jamii yao naye hayuko tayari kufanya hivyo.

Haraka, suala hili linakuwa jambo la kuvitia kwa Bibi Biyela-Ana uhakika litavuta usikivu wa wanafunzi wake na kuwapa uelewa zaidi wa utamaduni wa kuhadithia hadithi.

Kwa hiyo anapanga kuleta chombo cha kurekodi/kinasa sauti ili amrekodi Ma’Koku akihadithia hadithi, pamoja na kuongelea miiko ya kuhadithia mchana. Anajitahidi na kuhakikisha kuwa kikongwe huyu anaongelea suala hili namna ambayo wanafunzi wake wataelewa. Inavyoonekena, Ma’Koku ametatua tatizo lake kwa kuhadithia kinachowatokea watu wanaohadithia hadithi mchana.

Siku ya somo, Bi Biyela anakagua kinasa sauti chake na anahakikisha kuwa kote kote kiko sawa. Anatoa utangulizi wa somo, anawauliza wanafunzi kama wamewahi kusikia hadithi zilizotolewa na watu. Watoto wanahamasika -wanamsikiliza Ma’Koku akihadithia hadithi.

Baadaye, Bibi Biyela anaendesha majadiliano kuhusu kwa nini Ma’Koku hakuja kuwahadithia hadithi shuleni asubuhi ile. Anashangazwa na ukweli kwamba wanafunzi wengi wanaijua desturi ya kutohadithia mchana. Kufikia mwishoni wa kipindi, walikuwa wamejenga uelewea mkubwa wa mila na miiko inyohusiana/ambatana na suala hili.

Shughuli ya 1: Kuchagua hadithi murua/inayopendwa

Kabla ya somo, muulize kila mwanafunzi kuamua hadithi fupi aipendayo ili ashirikishe wenzake darasani.

Liandae darasa katika makudi madogo madogo ya watu kati ya wane hadi sita. Mtake kila mwanafunzi kuwahadithia hadithi yake kwenye kundi lake. Kabla hawajaanza, sisitiza kuwa kila mmoja apate nafasi ya kuhadithia pia wasikilize hadithi za mwenzao.

Baada ya hapo, waambie kila kundi kuchagua hadithi moja kutoka kwenye makundi yao. Hizi wataziwasilisha darasani. Kama ukigundua kuwa kuna kundi lolote linapata shida ya kukubaliana, ingilia kati kuwasaidia wachague hadithi.

Wape nafasi vikundi wajiandae. Ikiwezekana, andaa, mavazi, zana, midoli, vifaa vya muziki, n.k. au waambie wanafunzi wavilete, ili kufanikisha hadithi zao na kuwasaidia kufikisha ujumbe/maana.

Kila kundi liwasilishe hadithi yao kwa darasa zima na kufafanua kwa nini wanaipenda.

Hatimaye, jadiliana na darasa lako sehemu muhimu za hadithi, mwanzo? Hadithi yenyewe, mtiririko wa visa, mandhari, wahusika na mwisho/tamati.

Ulishangazwa na hadithi ambazo wanafunzi wako walichangua? Ni vizuri kiasi gani wanafunzi wako walifanya kazi pamoja katika makundi madogo? Je, unahitaji kupanga makundi tofauti kazi ijayo?

Sehemu ya 5: Sanaa ya kuhadithia hadithi