Nyenzo-rejea ya 1: Sauti ya kiwavi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Hapo zamani za kale, kiwavi kilitambaa hadi ndani ya nyumba ya sungura, wakati sungura akiwa hayupo, na kukaa kwa raha zake. Sungura aliporudi, aligundua alama mpya ardhini pangoni mwake. Aliita

‘Nani yuko ndani ya nyumba yangu? Kiwavi akalipuka kwa sauti kubwa, “Ni mimi! Ndiyo, ni mimi ninaye sagasaga kifaru hadi ardhini na kukanyaga tembo kwenye vumbi”.

Sungura akanyong’onyea na kulia akisema, ‘kiumbe mdogo kama mimi atamfanya nini kiumbe anayesagasaga kifaru na kukanyaga kanyaga tembo?’

Punde alikutana na mbweha na kumuuliza/kumwomba aongee na kiumbe huyo wa kutisha aliyejitwalia mji wake (sungura) ili amshawishi kuoondoka. Mbeha alikubali, na walipolifikia eneo alibweka kwa nguvu na kusema ‘Nani yuko ndani ya nyumba ya rafiki yangu Sungura?’

Kiwavi akajibu kwa sauti iliyotetemesha nchi, ‘Ni mimi! Ndiyo, mimi ninaye sagasaga kifaru hadi ardhini na kukanyagakanyaga tembo mavumbini!’ Alivyosikia haya, mbweha akafikiri ‘kwa vyovyote siwezi kufanya chochote juu ya kuimbe hicho,’ akaondoka mbiombio.

Sungura akamleta chui, na kumwomba amsaidie. Chui akamhakikishia kuwa hakutakuwa na tatizo. Alipofika kwenye tukio, chui alikwaruza kwa kucha zake na kusema, ‘Nani yuko ndani ya nyumba ya rafiki yangu sungura?’ Kiwavi alimjibu katika hali aliyowajibu wawili waliopita. Chui alihadharishwa na kufikiri, ‘kama kusagasaga kifaru na kukanyagakanyaga tembo, sitaki hata kufikiri atakachonifanya!’

Kilichofuata sungura akamwona kifaru. ‘Bila shaka, ni mnyama mwenye kutisha,’ kifaru alijigamba. Kifaru alitembea kwenda kwenye pango la sungura, alipokoroma na kuparura ardhi kwa miguuyake mizito.

Lakini kifaru alipouliza aliyeko ndani na kusikia sauti ya kutisha ya kiwavi, akafikiri ‘Nini, anasema anaweza kunisagasaga ardhini?’ Na kifaru akatoweka, akitokomea msituni.

Akiwa amekata tamaa, Sungura akamjaribu tembo kwa kumwomba masaada wake. Lakini kama wengine, aliposikia maneno ya kiwavi tembo akajua kuwa hakuwa anatamani kukanyagwakanyagwa kama mavumbi, akaondoka zake.

Kwa kusikitishwa na hoja hii, Sungura alimwomba chura aliyekuwa anapita kama anaweza kumsaidia na kumfanya kiumbe aliyowatisha wanyama wote aondoke nyumbani mwake. Chura alikwenda kwenye mlango wa pango na kuuliza aliyekuwa ndani. Alipokea jibu lilelile walilopewa wengine. Kisha chura alisogea karibu na kupiga kelele, ‘Mimi niliye na nguvu kuliko wote, nimekuja hatimaye. Mimi husagasaga wale wasagao vifaru! Mimi huwakanyagakanyaga tembo!’

Kiwavi aliposikia hayo kule ndani alitetemeka. Alihisi kivuli cha chura kikisogea na kufikiri, ‘Hata hivyo mimi ni kiwavi tu! Na kiwavi akajificha kwenye tundu lililokuwa kwenye pembe ili asionekane. Wanyama waliokusanyika karibu na nyumba ya sungura walimkamata na kumtoa nje. ‘Nani, wewe?’ Wote walipiga kelele kwa kutoamini.

‘Siwezi kufikiri kukaa ndani ya pango hilo!’ Kiwavi aliyasema pua akawa amebinua juu, ‘mwangwi wake anatisha kwa kiumbe mungwana kama mimi!’ Alivyo ondoka zake, wanyama wengine wakacheka kwa matatizo/usumbufu aliowasababishia.

Nyenzo-rejea ya 2: Hadithi na hekaya kutoka Afrika