Nyenzo-rejea ya 2: Hadithi na hekaya kutoka Afrika

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Tovuti hapa chini imekupa zaidi ya hadithi 50 na ngano katoka Afrika http://www.gateway-africa.com/ stories/ [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)]

Kama hii hapa chini

Radi na mwale wa radi

Hapo zamani za kale radi na mwale waliishi hapa duniani pamoja na watu. Radi alikuwa kondoo jike na mwale ulikuwa mtoto kondoo dume. Hakuna mnyama aliyekuwa maarufu kwa watu, kwani pale mtu alipomkosea mwale, angepaa kwa ghadhabu na kuanza kuunguza chochote alichokutana nacho. Hii ilihusisha vibanda, vihenge na hata miti

mikubwa. Wakati mwingine angeharibu mazao shambani kwa moto wake na muda mwingi aliua watu waliopita kwenye anga zake. Radi alipojua kuwa wanae alikuwa na tabia ya aina hii, aliinua sauti na kumpigia kelele na zilikuwa kilele kweli kweli. Kiuhalisia, majirani walikuwa wamehuzunishwa, kwanza kwa hasara, iliyosababishwa na mwale na kwa sauti zisizovumilika zilizotoka kwa mama yake zilizokuwa zinafuatia upasukaji wake. Wanakijiji walilalamika kwa mfalme matukio mengi hadi pale alipowaagiza wote wawili kuishi kwenye mpaka wa kijiji na kuwaambia kuwa wasjie wakachanganyika tena na watu. Hata hivyo, hii haikusaidia kwani mwale aliendelea kuwaona wanakijiji walipokuwa wakitembea kijijini/Mitaani hivyo kupata urahisi wa kuendelea kukwaruzana/kuzozana nao.

Mfalme akawatumia ujumbe tena aliwaambia ‘Nimewapa fursa nyingi kuishi maisha mazuri, lakini naona kuwa haijafaa chochote. Kuanzia sasa na kuendelea, mwende mbali na kijiji chetu, mkaishi kwenye pori. Hatutaki kuona sura zenu hapa tena.’ Radi na mwale iliwabidi watii mfalme na kukubali kufuata hukumu yake. Hivyo waliondoka kijijini, wakiwa na hasira na wakazi wake. Bado kulikuwa na matatizo makubwa kwa hifadhi za wanakijiji, kwani mwale alikasirika kwa kufukuzwa kiasi

kwamba aliwasha moto kwenye pori lote, na kwa vile ilikuwa wakati wa kiangazi, hali hii ilikuwa mbaya zaidi.

Moto aliambaa kwenye mashamba madogo ya watu na wakati mwingine kwenye nyumba zao, sasa walikuwa kwenye mashaka tena. Mara nyingi walisikia sauti ya kondoo jike (mama wa kondoo dume) akimwita mwanae akimuonya aache lakini kwa vile aliyafanya baada ya tukio, haikuleta tofuati yoyote. Mfalme aliwaita washauri wake ili wamshauri. Baada ya mdahalo mkubwa, wakapata mpango. Kwa nini tusiwafukuze radi na mwale jumla watoke duniani, na kuwasukumia kuishi angani? Hivyo mfalme akaafiki. Radi na mwale walitupwa/sukumwa angani ambapo

watu walitumainia kuwa hawasabisha madhara tena.                                                                Lakini mambo hayakwenda kama walivyotarajia; hata hivyo mwale bado anaonyesha hasira yake mara kwa mara na hawezi kuacha kutupa moto duniani anapokasirika. Unaweza kumsikia mama yake akimkemea kwa sauti yake ya kutisha.

Imepatikana katika chanzo: Gateway Africa, Website

Nyenzo-rejea ya 1: Sauti ya kiwavi

Nyenzo-rejea ya 3: Picha za hadithi