Nyenzo rejea 4: Kutumia picha kama kichokoo cha kuandika hadithi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi

Picha zinaweza kuwa kichokoo kizuri cha uandishi wenye ubunifu kabla wanafunzi hawajaandika hadithi au ushairi wao. Unaweza kuijadili picha iliyochaguliwa na darasa zima au uwe na makala nyingi za sura hiyo hiyo au sura tofauti ili wanafunzi wajadiliane katika makundi yao. Kama una darasa kubwa unahitaji kuwa na sura nyingi au ufanye kazi na nusu darasa kwa wakati mmoja wakati wengine wakifanya kazi nyingine.

Maswali yafuatayo yanaweza kutumika pamoja na picha yoyote ili kuchokoa mawazo na ubunifu. Unaweza kuandika maswali ubaoni na kuyajadili na darasa zima au lipe kila kundi maswali yake na waambie watoe majibu ndani ya muda mfupi/dakika chache. Baadhi ya maswali hayatafaa kwa kila picha. Itabidi uchague yale yanazoendena na malengo au waambie wanafunzi kuibua maswali juu ya picha.

1.       Unafikiri kinatokea nini kwenye picha hii?

2.       Unafikiri inaitwaje?

3.       Nini kinakuvutia kwenye picha hii? Kwa nini?

4.       Unapenda nini kwenye picha hii?

5.       Hujapendezwa na nini kwenye picha hii?

6.       Kuna hadithi gani kwenye picha hii?

7.       Nini/kipi kilisababisha picha hii ipakwe rangi/picha hii ichukuliwe?

8.       Unafikiri nini kitatokea baadaye?

Nakili majibu ya wanafunzi ubaoni ili wayatumie ukiwapa kazi ya kuandika hadithi; lakini wahamasishe kuwa wabunifu na kutumia mawazo yao.

Wahamasishe kufikiri kilichotokea hapo kabla ya picha na ikiwezekana waanzie hadithi yao pale.

Nyenzo-rejea ya 3: Picha za hadithi