Kuna vitengo 15 vya Sayansi ya Sekondari vya TESSA ambavyo unaweza kuvipata katika ukurasa huu.
Vimeundwa na washiriki kutoka Ghana, Zambia, Kenya, Tanzania na Uganda.
Tumechagua mada ambazo ni ngumu kwa kufundisha kutokana na mtaala wa Sayansi ya Sekondari ya awali na pia zilizo za kawaida katika nchi zote.
Vitengo vimekusanywa katika makundi matano ya dhamira za ufundishaji, yakionyesha ufundi na tabia ya mwalimu mwenye ufanisi.
Hivi ni:
- Kuchunguza kwa makini uelewaji wa wanafunzi
- Kuifanya sayansi ya utendaji
- Kuifanya sayansi ya ukweli na yenye maana
- Kutatua masuala na ubunifu
- Kufundisha mawazo yenye changamoto
Kila dhamira hujitokeza kwa mfano wake katika Biolojia, Kemia na Fizikia, na zote huwa jumla ya vitengo 15.
Kama mada unayoifundisha haikuwekwa humu, basi tunatumai kwamba wewe mwenyewe utaweza kuirekibisha mojawapo ya vitengo ili vilingane na hali halisi ya kile unachokihitaji.
Kama ungependelea kuchagua dhamira ya ufundishaji mmoja tu basi itakubidi kupakua sehemu zote za 1 ili kujifunza jinsi ya ‘kuchunguza ufahamu wa watoto’; sehemu ya 2 ili kujifunza jinsi ya ‘kuifanya sayansi ya utendaji’; sehemu ya 3 ili kujifunza jinsi ya ‘kuifanya sayansi ya ukweli na yenye maana’; sehemu ya 4 ni kujifunza jinsi ya ‘kutatua masuala na ubunifu’; na sehemu ya 5 ni kujifunza jinsi ya ‘kufundisha mawazo yenye changamoto’.
Kama rasilimali hizi ni inapatikana kwa Kiingereza utaelekezwa kwa pan-Afrika toleo English