Nyenzo-rejea 2: Orodha ya kuhakiki kwa ajili ya wanafunzi - ili kutumika wakati wanapohariri kazi zao kwa ajili ya kitabu
Kwa ajili ya matumizi ya mwanafunzi
Orodha ya kuhakiki hadithi | |
Hadithi ina kichwa cha habari? | |
Je, Kichwa cha habari hicho kitawafurahisha wasomaji wa hadithi? | |
Je, wasomaji wataweza kufuata mtiririko wa matukio katika hadithi (ilitokea nini kwanza halafu kilichofuata ni nini)? | |
Je, Wahusika na mandhari katika hadithi vimeelezwa vizuri ili wasomaji waweze kupata taswira yavyo? | |
Je, hadithi inafikia upeo/mwisho? | |
Orodha ya kuhakiki mashairi | |
Shairi au wimbo una kichwa cha habari? | |
Je, kichwa cha habari hicho kitawafurahisha wasomaji wa mashairi au wimbo? | |
Je, shairi au wimbo una wizani au vina (au vyote viwili) ambavyo vinawafanya wasomaji wafurahie? | |
Maneno yameteuliwa vyema kuelezea watu, wanyama, vitu, matendo au hisia? | |
Orodha ya kuhakiki michezo | |
Je, mchezo una jina? | |
Je, maelekezo yana mtiririko sahihi? (kwanza fanya hili ……) | |
Je maelekezo yako wazi? | |
Iwapo vitu (kama changarawe au karatasi) vinahitajika katika mchezo, je, vimeorodheshwa? |
Nyenzo-rejea 1: Jinsi hadithi zinavyoandikwa kuwa vitabu