Sehemu ya 3: Kuunda Fursa za Mawasiliano
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuunda shughuli za kukuza mawasiliano katika lugha ya ziada?
Maneno muhimu: tofauti katika taarifa; maingiliano ya kimawasiliano; umaanifu; kuunda shughuli; makundi
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- umeunda shughuli za mawasiliano halisi katika darasa lako la lugha ya ziada;
- umeendeleza ‘maktaba’ ya nyenzo za kuchochea mazungumzo asilia;
- umetumia kazi za vikundi na za wanafunzi wawili wawili ili kukuza mawasiliano ya lugha ya ziada.
Utangulizi
Ukiwa mwalimu, unapaswa kutumia matokeo ya tafiti kuhusiana na kitu unachokifanya. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kwamba watu hujifunza lugha kutokana na kushiriki katika mawasiliano yenye maana ya lugha husika, katika mazingira asilia. Hoja hii inamaanisha nini?
‘Kushiriki’: Kila mwanafunzi lazima ashiriki –au ahusishwe kikamilifu.
‘Umaanifu’: Shughuli lazima iwe inalandana na mazingira halisi na ilete maana kwa wanafunzi.
‘Maingiliano’: Mawasiliano lazima yahusishe njia-mbili (au njia tatu au nne).
‘Mazingira asilia’: Lugha inayotumiwa lazima iwe lugha ya kawaida ya mawasiliano ya kila siku.
Katika sehemu hii, tunaangalia jinsi ya kuchochea maingiliano ya kimawasiliano ya aina hii darasani kwako, hususan kwa kutumia picha. Tunashauri kwamba uunde uteuzi wa zana.
Kwa kawaida, darasa lenye kazi za maingiliano ya kimawasiliano hufanywa katika makundi madogo madogo. Itasaidia kusoma Nyenzo-rejea Muhimu: Kutumia kazi za vikundi katika darasa lako .
Nyenzo-rejea 5: Vitenzi na vielezi katika shairi – Ngoma Yangu na Francis Faller