Sehemu ya 5: Vitendo vya kuimarisha ustawi wa kiroho
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kupanga shughuli za wanafunzi zinazoimarisha ustawi wao wa kisaikolojia?
Maneno muhimu: mwelekeo chanya; utoaji hadithi; shughuli za shule nzima; ustawi wa kiroho
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- Kugundua njia za kuimarisha mwelekeo chanya darasani
- Kutumia mbinu ya kutoa hadithi na majadiliano ili kuwasaidia wanafunzi kujihisi salama.
- Kugundua tabia mbalimbali za wanafunzi binafsi ili kuwasaidia kujifunza zaidi;
- Kupanga shughuli za kusherehekea maisha pamoja na darasa zima na shule kwa ujumla.
Utangulizi
Kuimarisha ustawi wa kiroho kwa wanafunzi wako ina maana ya kuwafanya wawe na furaha na wawe wametulia katika maisha yao ya kila siku, na wawe na amani wao kwa wao na wenzao. Ustawi wa kiroho unahusisha vipengele vya maisha yote ya wanafunzi, ikiwa ni pamoja na maisha ya kimwili na kihisia.
Katika sehemu hii, tutazingatia vipengele vinavyohusiana na ustawi wa kiroho na jinsi ya kupanga shughuli ambazo zitasaidia ustawi huo. Unapaswa kujua ni mambo gani yanayowatia hofu au yanayowaondolea mashaka, na kuyashughulikia katika madarasa yako. Tunapendekeza kusimulia hadithi na shughuli za shule nzima katika ujenzi wa ustawi wa kiroho.
Nyenzo-rejea 2: Tafakuri ya mama Msekwa kuhusu mkabala wake