Namba ya moduli 2: Kutalii Maendeleo ya Jamii
Sehemu ya 1: Kutambua mtandao (muingiliano) wa jamii
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kugundua mtandao wa jamii kwa kutumia igizo kifani, michoroti ya familia na wataalamu wenyeji?
Maneno muhimu: igizo kifani; tofauti; kutatua tatizo; madarasa makubwa, mtandao wa kijamii, michoroti ya familia.
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- Kuanzisha majadiliano na kutumia michoroti ya familia kubainisha wana-familia wa karibu na wa mbali wa wanafunzi;
- Kutumia igizo kifani na mbinu ya utatuzi-matatizo kutalii mtandao na mahusiano katika shule;
- Kufanya kazi na wataalamu wenyeji ili kuboresha maarifa ya wanafunzi kuhusu mitandao ya kijumuiya.
Utangulizi
Watoto wanatoka katika familia, koo, makabila na jumuiya nyinginezo mbalimbali zinazowatambulisha wao ni kina nani. Ukiwa mwalimu, unahitaji kuwa makini na tofauti hizi na kujitahidi kuwajumuisha wanafunzi wako katika makundi yote haya katika jitihada za kuwa na mitandao mikubwa zaidi.
Katika sehemu hii, utatumia mbinu mbalimbali za ufundishaji na Nyenzo-rejea ili kuwasaidia wanafunzi wako kutambua mahusiuano yaona kuheshimu tofauti zao. Tunaanza na majadiliano na kuchora mchoro wa miti wa familia uoneshao mahusiano ya kifamilia. Utatumia shughuli za igizo kifani na mbinu ya utatuzi-matatizo ili kuwasaidia wanafunzi kutambua mahusiano yao ya kifamilia shuleni.
Mwisho, tunakushauri kuwa umkaribishe mtaalamu kutoka katika jumuiya ili aelezee mahusiano ya kifamilia makubwa zaidi ambayo huunda sehemu ya maisha ya wanafunzi.