Namba ya moduli 2: Utafiti wa Kihistoria

Sehemu ya 1: Utafiti wa historia ya familia

Swali Lengwa muhimu: Namna gani unaweza kupanga shughuli vikundi vidogo vidogo darasani kukuza ufanyaji kazi pamoja na kujenga kujiamini?

Maneno muhimu: familia: historia: kujiamini: utafiti: kundi dogo la kazi: majadiliano.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umepanga kazi zako kusaidia wanafunza kujielewa wenyewe na uhusiano wao na familia nyingine;
  • umetumia makundi madogo ya majadiliano kujenga kujiamini wanafunzi wakiwa wanatafiti historia za familia zao.

Utangulizi

Ufundishaji mzuri huanza kwa kuwahamasisha wanafunzi kutafiti mambo ambayo wanayafahamu.Kihistoria, hii ina maana kutumia maisha yao na ya familia zao kama chanzo cha utafiti. Ujuzi uliotumika kutafiti historia ya familia, unaweza kutumika kutafiti masuala mapana zaidi ya kihistoria.

Sisi wote tuna historia,iliyoanza mara baada ya kuzaliwa.Hii inajumuisha uzoefu wetu na watu wote tunaohusiana nao.

Katika sehemu hii,unaanza kutafiti hali za familia za wanafunzi wako, kazi na majukumu yao katika famlilia zao. Utaangalia pia kwa upana familia kubwazenye misingi ya kiukoo. Kadili unavyotafiti sehemu hii unatakiwa kuwa makini na uzoefu tofauti wa familia au miundo mingine ambayo wanafunzi wako wanaiishi.