Namba ya moduli 3: Kuchunguza vipimo na Kusimamia
Sehemu ya 1: Kuwasilisha vipimo
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutambua elimu ya awali ya wanafunzi juu ya vipimo, na kupanga shughuli za vitendo kuendeleza uelewa huo?
Maneno muhimu: kupanga, kipimo, mapigo ya moyo, elimu ya awali, zana; ramani ya mawazo
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- Umetumia ramani ya mawazo kutafuta wanafunzi wanachofahamu tayari juu ya kipimo na kupima;
- Umetumia ufundishaji wa mtaala mtambuka kuona jinsi maeneo ya somo yanavyoingiliana;
- Umepanga masomo yako kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika kukuza uelewa wao wa kupima.
Utangulizi
Tunapima vitu vingi katika maisha yetu ya kila siku, kama vile urefu, uzito wa mboga zetu, umbali tuliotembea.
Ni mifano gani ya kipimo ungetegemea wanafunzi wako waifahamu? Bila seti za darasani za vifaa vya kupimia, ni vipi wanafunzi wako wanaweza kufanya kazi na data halisi za kiasi, ili waelewe ni wapi namba zinatokea na zina maana gani? Na unawasaidiaje kupata maana ya viambishi awali kama ‘mega-’ na ‘mili-‘? Sehemu hii itakusaidia kuchunguza mambo haya yote.