Somo la 2
Tupendayo na tusiyoyapenda yanaweza kuathiri jinsi tunavyojifunza. Shughuli tuipendayo hutupa motisha, wakati shughuli ambayo hatuipendi inaweza kuzuia kujifunza.
Hisia na hulka za wanafunzi zinaathiri sana namna tunavyovutika katika shughuli mbalimbali. Baadhi ya wanafunzi wana aibu sana na hawawezi kuzungumza mbele za watu, wakati wengine hupenda kutenda. Baadhi ya wanafunzi hupenda kufanya kazi peke yao, wakati wengine hufanya vizuri zaidi wakiwa katika makundi. Wengine hupenda kujifunza kwa kusoma, wakati wengine hujifunza zaidi kwa kuzungumza.
Unapaswa kung’amua wanafunzi wako wanapendelea au hawapendelei shughuli ipi ili kukusaidia kupanga somo lako vizuri. Hali hiyo itakidhi haja yao ya ustawi wa kiroho ambao utawafanya wajifunze vizuri zaidi.
Uchunguzi kifani ya 2: Upangaji wa kuhimiza ustawi wa kiroho
Mwalimu Agasso aliorodhesha mbinu mbalimbali za kutumia katika masomo yake baada ya kujadiliana na wanafunzi wake jinsi ya kujihisi salama:
- Wanafunzi wengi hufurahia kucheza na wenzao. Hivyo michezo ya makundi itumike mara kwa mara.
- Baadhi ya wanafunzi wengine walipendelea kufanya kazi kimyakimya. Hivyo aliamua kutoa nafasi ya kufanya kazi kipekee pekee kama katika shughuli za kusoma, kuandika, na kuchora.
- Wanafunzi walipendelea kuimba na muziki. Hivyo aliamua kutumia nyimbo kuwahamasisha na kuwafurahisha.
- Hakuna mwanafunzi aliyependa kutishwa. Hivyo anapaswa kuwa mwangalifu kuhusu hali ya kukasirika darasani. Anapaswa pia kuzingatia tabia ya baadhi ya wanafunzi darasani ambao ni watetezi wa kupita kiasi au watumizi wa maguvu
Mwalimu Agasso alizingatia hali ya baadhi ya wanafunzi darasani na aliwaangalia kwa makini wakati wakifanya kazi. Aliwaangalia jinsi kila mmoja alivyochukulia shughuli mbalimbali.
Alitumia taarifa hizi kutayarisha masomo yake ambao yalihusisha shughuli za kufanya kila mmoja peke yake na za kufanya katika makundi. Alitayarisha makundi ili kuhakikisha kuwa:
- Hakuna aliyetengwa;
- Hapakuwa na mgongano wa haiba;
- Kila mmoja alichangia mawazo; na
Kila mmoja alifurahia kufanya kazi na mwenzie.
Shughuli ya 2: kutambua haiba ya wanafunzi wako
Fikiria haiba mbalimbali za wanafunzi wako darasani na jinsi wanavyoshiriki katika njia utumiayo kufundisha. Jiulize:
- Ni wanafunzi gani ambao hujibu maswali mara nyingi;
- Ni wanafunzi gani wasioongea darasani;
- Utaielezaje haiba yao;
- Ni wanafunzi gani hufanya vizuri katika makundi;
- Ni wanafunzi gani hufanya vizuri wakiwa peke yao;
- Ni wanafunzi gani huonesha tabia mbaya katika makundi;
- Ni wanafunzi gani hupata shida wakifanya kazi peke yao;
Sasa fikiria shughuli unaztumia:
- Ni shughuli gani zinapendwa zaidi;
- Ni shughuli gani zisizopendelewa zaidi;
- Ni shughuli gani husaidia wanafunzi kujifunza vizuri zaidi;
Linganisha wanafunzi na aina ya shughuli zinazowafaa.
Utapangaje shughuli mbalimbali ili kila mwanafunzi afaidike?
Andaa somo kwa kutumia mawazo haya. Fundisha somo hilo na kisha fikiri:
- Maoni yako yalikuwa sahihi
- Wanafunzi walifanyaje katika somo hilo; na
- Utalibadilishaje wakati mwingine.
Somo la 1