Somo la 3
Soma Nyenzo rejea 1: Sherehe.
Unapowasaidia msaada chanya wanafunzi wako, unawasaidia kusherehekea mafanikio yao. Hii inaweza kujumuisha:
- Kutambua ufanisi na mafanikio yao;
- Kutambua stadi na kipaji chao;
Wanafunzi hufanya vizuri zaidi wanapopata msaada chanya. Unaposherehekea mafanikio yao:
- Unawatia moyo;
- Unawahamasisha kufanya vizuri zaidi; na
- Unawasaidia kuboresha hali ya kujithamini na kujiamini.
Sherehe sio lazima iwe kubwa. Hata kusema ‘Umefanya vyema’ kwa mwanafunzi ni sherehe ndogo na huwezesha msaada chanya kama ilivyoelezwa hapo juu.
Unaweza pia kusherehekea kama darasa au shule kwa ujumla.
Sehemu inayofuata inahusu namna ya kusaidia kusherehekea stadi na vipaji. Vitu vya kusherehekea sio lazima viwe vya stadi za kitaaluma tu, bali pia vitu ambavyo wanafunzi wanavimudu au wanafurahia kuvifanya nje ya shule.
Unaposherehekea vitu hivyo, unaonesha kuwa shule:
- Inatambua vipaji mbalimbali walivyonavyo wanafunzi wako;
- Inawaunga mkono wanafunzi wako katika vipengele vingine vya maisha yao.
Hali hiyo itawatia moyo wanafunzi wako kujihisi kuwa shule ni mahali ambapo wanapatamani na kupaheshimu kwa njia mbalimbali.
Uchunguzi kifani ya 3: Upangaji wa mchezo wa kuigiza
Wakati wa mapumziko, mwalimu Damas aligundua kwamba, wanafunzi wengi walicheza michezo iliyohusu kuimba na kucheza muziki. Aliona kuwa angetumia mbinu hii katika ufundishaji wake. Alimwomba mkuu wa shule kumruhusu darasa lake lijitayarishe kufanya onesho la kuigiza. Wanafunzi walifurahi sana.. Alitumia utaratibu ufuatao katika kupanga onesho hili:
- Alijadiliana na darasa lake wangependa igizo hilo liwe juu ya nini.
- Wakiwa katika makundi wanafunzi walijadili vitu mbalimbali ambavyo wangeviingiza katika igizo hilo katika kipindi cha dakika 15 walizopewa.
- Kama darasa waliamua kukusanyika na kufanya onesho lililohusu kushirikiana. Walitayarisha onesho fupi, mchezo mfupi na wimbo na dansi. Ilikuwa muhimu kuchagua shughuli ambayo ingewahusisha wanafunzi wengi kwa kadri iwezekanavyo.
- Baadhi ya wanafunzi hawakupenda kujihusisha na onesho lakini mwalimu Damas aliwahusisha katika kutengeneza nguo za maonesho au kushiriki kama papo kwa hapo.
- Wakati wakitayarisha shughuli zao, mwalimu Damas alikagua kuhakikisha kama kila mmoja alikuwa anajua analolifanya. Wanafunzi hawakulazimishwa kuzungumza hadharani ila kwa kutaka kwao.
Waliigiza mbele ya darasa zima. Igizo hilo lilikuwa zuri na kila mmoja alilipenda. Mwalimu mkuu aliamua kufanya shughuli hii kuwa jambo la kila mara, kila darasa likiwa na zamu yake ya kufanya igizo kwa shule nzima au kuonesha waliojifunza. Lilikuwa jambo zuri la kuendeleza hali ya kujiamini kwao na kujithamini.
Soma Nyenzo rejea: Matumizi ya michezo ya kuigiza/mazungumzo/ drama darasani ili kupata mawazo zaidi
Shughuli muhimu: Upangaji wa sherehe
Ili kuwasaidia wanafunzi wako kupanga sherehe inakubidi pamoja nao uzingatie vipengele mbalimbali kwanza.
Waulize, katika makundi yao, wakutajie matukio mbalimbali wanayosherehekea. Waombe waorodheshe shughuli mbalimbali wanazofanya wakati wa sherehe.
Pambanua pamoja na wanafunzi tukio linaloweza kusherehekewa shuleni.
- Waombe wapange shughuli za tukio hilo - shughuli, michezo, nyimbo n.k. Hakikisha kuwa kila mmoja amehusika kwa namna moja au nyingine, hata kama hawatatenda. Wasaidie kufanya mazoezi.
- Darasa likiwa tayari, fanya igizo hilo kwa darasa lingine au shule nzima. Ungeweza kuwakaribisha wazazi na wanakijiji/wanajamii.
- Siku inayofuata waombe wanafunzi wako kuandika maelezo kuhusu yote waliyofanya katika kujitayarisha kufanya sherehe hiyo. Waulize wapambanue stadi mpya walizojifunza. Waulize wanapenda kusherehekea nini wakati ujao.
- Je, wamefanikiwa?
- Unajuaje?
Wanafunzi wameshughulika vipi?
Somo la 2