Nyenzorejea ya 4: Kujiandaa kwa matembezi ya kijumuiya – kipindi hicho wanafunzi watagundua chapa za kimazingira
Nyenzo Rejea ya mwalimu kwa kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
Hatua 1: Kama darasa lako ni kubwa sana, unaweza kuwaomba watu wazima kutoka kwenye jumuiya wakusaidie kufanya matembezi na vikundi vya wanafunzi. Kama unawaomba, kutana nao kabla ya matembezi kuwaeleza kile unachotaka wao wafanye. Lazima wajue ni maswali gani utawauliza wanafunzi na ni mifano gani ya chapa za kimazingira unataka wanafunzi wazigundue. Wanaweza pia kuwa na mapendekezo ya kukupa.
Hatua 2: Panga shughuli kwa kutembelea mazingira yote yanayoizunguka shule yako. Kwa baadhi yenu eneo hili linaweza kuwa ni kijiji, kwa wengine sehemu ya jiji lenye shughuli nyingi. (Angalizo: Kama shule yako ipo sehemu ambayo imejitenga, unaweza kuhitaji kusaidiana na wanajumuiya ili kupanga usafiri wa wanafunzi kwenda sehemu ambayo wanaweza kuona chapa mbalimbali za kimazingira). Angalia kila mfano wa chapa ya kimazingira unaoweza kuwavutia wanafunzi na panga njia ambayo wewe na wanafunzi mtapitia wakati wa matembezi. Aina za chapa na maumbo/picha, kwa hakika, itatofautiana sana kutoka kwa eneo jirani moja na jingine lakini zinaweza kujumuisha majina (mf.shule, kliniki, msikiti, kanisa, ukumbi wa jumuiya, duka, mto, mtaa); alama (mf. Alama ya SIMAMA); matangazo kwenye mabango makubwa au kwenye kuta za maduka; taarifa za kijumuiya (mf. mabango ya uchaguzi au taarifa kuhusu mikutano au matukio ya kijamii au michezo).
Hatua 3: Andaa orodha ya maswali watakayoyajibu wanafunzi. Haya yanaweza kujumuisha:
Alama au jina hili linatuambia nini?
Unafikiri kwa nini limewekwa hapa?
Limeandikwa kwa lugha gani?
Unafikiri kwa nini limeandikwa kwa lugha hii?
Unapata taarifa gani kutokana na mchoro au picha kivuli hii unayoiona?
Ni alama ipi ambayo ni rahisi kuisoma? Kwa nini?
Unapenda alama ipi? Kwa nini?
Unawezaje kuboresha baadhi ya alama hizi?
Ni majina gani mengine, alama, matangazo, mabango, taarifa ambazo ungependa kuwa nazo katika mazingira ya hapa jirani? Kwa nini ungependa kuwa nazo hizi?
Nyenzorejea ya 3: Maswali ya mfano ya kuuliza kuhusu bidhaa za dukani