Nyenzo-rejea ya 1: Uulizaji wa maswali – kuwahimiza wanafunzi kufikiri kwa umakinifu kuhusu hadithi
Nyenzo ya Mwalimu kwa ajili ya kupanga/kurekebisha na kutumia na wanafunzi
Mfano A: Hadithi kuhusu familia
Unaweza kuuliza maswali kama:
Ni wanafamilia wapi waliomo katika hadithi?
Wapi wanaonekana muhimu? Unawatambuaje?
Je, familia yako inafanana na hii? Kama hivyo ndivyo, kwa njia zipi? Kama sivyo, inatofautianaje?
Wanafamilia wanafanya nini? Je, watu katika familia yenu wanaweza kuwa na mwenendo kama huo?
Unafikiri mwandishi anataka watu waamini nini kuhusu familia?
Mfano B: Hadithi iliyotayarishwa shuleni
Unaweza kuuliza maswali kama:
Shule katika hadithi inafanana na shule yetu?
Ni kwa njia zipi majengo yanafanana? Ni kwa njia majengo ni tofauti?
Ni kwa njia zipi watu - mwalimu mkuu, walimu, wanafunzi - wanafanana na wale wa shuleni kwetu? Ni kwa njia zipi wanatofautiana?
Je, watu katika hadithi wana mwenendo au wana matendo kama watu wa shuleni kwetu au wana mwenendo au wanatenda tofauti? Toa mifano kuthibitisha jibu lako.
Unafikiri mwandishi katika hadithi anawataka wasomaji kuamini nini kuhusu shule?
Angalizo: Unaweza kuuliza maswali kama haya kuhusu kijiji, mji, jiji ambapo hadithi kama hii inatolewa. Lengo ni kuwafanya wanafunzi kulinganisha kati ya yale wanayoyajua na wanayosoma juu yake.
Somo la 3