Nyenzo-rejea ya 4: Kutengeneza matangazo
Nyenzo-rejea ya Mwalimu kwa ajili ya kupanga/kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
Tathmini ya mwitiko wa wanafunzi katika kujibu maswali yanayohusu matangazo.
Tumia maswali haya kutathmini kazi za wanafunzi:
- Kuna ushahidi kuwa wanafunzi wameelewa kazi waliyotarajiwa kuifanya? Kwa mfano, mwanafunzi amechagua/hakuchagua tangazo; mwanafunzi amejaribu/hakujaribu kujibu swali?
- Ni maswali yapi ambayo mwanafunzi amejibu kwa mafanikio zaidi? Kuna ushahidi upi unaoonesha kuwa majibu ni ya mafanikio?
- Ni maswali yapi ambayo mwanafunzi hakujibu vizuri au kwa usahihi? Ni kitu kipi kinakosekana katika majibu yake au ni makosa yapi yaliyomo katika majibu yake?
Masomo ya ufuatiliaji
Warudishie wanafunzi kazi zao na toa maoni ya jumla kuhusu kazi walizozifanya vizuri na ni mahali papi ambapo wangepaboresha zaidi.
Watake wanafunzi wafanye kazi katika vikundi vilevile kama walivyofanya katika somo la kujibu maswali kuhusu matangazo.
Kipe kila kikundi karatasi kubwa na, kama inawezekana, kalamu za kuchorea au rangi pamoja na brashi.
Watake wafikirie bidhaa mpya (k.m. aina ya chakula, gari, kifaa cha nyumbani, nguo) na wapange jinsi ambavyo wangechora au wangeandika tangazo. Wanatakiwa kufikiria juu ya maswali waliyojibu katika somo lililopita.
Watake wachore na kutengeneza tangazo la bidhaa hii mpya.
Nyenzo-rejea ya 3: Usomaji makinifu wa matangazo