Nyenzo-rejea 5: Maswali kwa ajili ya tathmini binafsi
Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu
Unapojibu maswali haya, ni muhimu uwe mkweli ili uweze kuwa mwalimu bora.
- Je, ninajiamini zaidi katika kutumia kazi za vikundi?
- Je, kutumia vikundi vyenye ukubwa tofauti na vya aina mbalimbali kumeboresha masomo yangu na kurahisisha welewa wa wanafunzi?
- Je, ninajisikia kama kazi za vitendo zimewasaidia wanafunzi kuelewa, na kujiamini?
- Je, wanafunzi wangu wanafurahia kufanya kazi hizi za vitendo za hisabati?
- Je, niliwapa wanafunzi wangu muda wa kutosha wa kufanya kazi zao za vitendo?
- Je, nitawezaje kuboresha ufundishaji wangu wa mada hii?
- Wakati ujao nitabadili kitu gani?
Maswali kuhusu utumizi wa kazi za vitendo na nyenzo rahisi
- Je, shughuli hizi zinanisaidia katika kutimiza malengo yangu ya ujifunzaji?
- Shughuli hizi zilikuwa zinafaa darasa langu?
- Je, shughuli hizi ziliamsha hamasa za wanafunzi?
- Je, nyenzo zilinisaidia kufikia malengo yangu ya ujifunzaji?
- Je, nyenzo zilikuwa zinalifaa darasa langu?
- Je, nyenzo ziliamsha hamasa za wanafunzi?
- Somo lilikuwa linafurahisha kwa kiasi gani?
Nyenzo Rejea 4: Kulinganisha namba sehemu