Nyenzo-rejea ya 1: Kukusanya na kutengeneza maumbo na violwa
Nyenzo ya Mwalimu kwa ajili ya kupanga/kurekebisha na kutumia na wanafunzi
Utahitaji kuchora/kutengeneza vipande vya kadibodi za maumbo ya P2 yafuatayo:
Pembetatu Mraba
Pentagoni/Pembetano Pembesita
Pembesaba
Pembenane
Sasa unaweza kuchunguza violwa vya P3
Vilevile, unahitaji kukusanya au kutengeneza violwa vya P3:
Tufe
Mchemraba (mfano, kibonge cha sukari, au mchemraba uliotengenezwa kutokana na njiti za kiberiti)
Miche mstatili (mfano, boksi la kiberiti, boksi la viatu)
Koni (unaweza kukata kutoka sehemu nyingine na kuchomeka kwenye wavu wa koni uliopo hapa)
Micheduara (vibiringisho vya karatasi za chooni, msokoto wa kipande cha karatasi kilichoshikishwa kwa gundi).
Aidha, unaweza kutengeneza michemiraba, mapiramidi au micheduara kwa kutumia karatasi au mirija.
Somo la 3