Nyenzo-rejea ya 4: Uhamishaji na uakisi wa pembetatu
Taarifa za msingi/ welewa wa somo wa mwalimu
*Uhamishaji wa pembetatu abc kwenda a1b1c1
Katika viwianishi x-y kwa kawaida thamani ya ‘x’ (mhimili ulalo)
hupatikana kabla ya thamani ya ‘y’ (mhimili wima).
Kwa hiyo, kwa ufafanuzi, viwianishi x-y vya abc ni:
a = 4, 8
b = 4, 2
c = 2, 2
Uhamishaji kwenda a1b1c1 unaongeza thamani ya x kwa 12, na y kwa 9. Kwa hiyo:
a1 = 16, 17
b1 = 16, 11
c1 = 14, 11
Upambanuzi
Huu unaweza kurahisishwa, kwa kutembeza umbo lililokatwa kuzunguka fito mraba, kwa kuchora kulizunguka umbo hilo na kuandika rekodi ya viwianishi vipya.
Hii inaweza kufanywa kuwa yenye changamoto zaidi kwa kutoa viwianishi vya umbo na kuwaambia wanafunzi wachore umbo hilo. Kisha, sema jinsi uhamishaji ulivyoathiri thamani za x na y, na waambie wanafunzi watafute viwianishi vipya na kuchora tena mwonekano wa umbo hilo.
*Uakisi wa pembetatu abc kwenda a, b, c
Katika ufafanuzi, viwianishi vya x na y vya abc ni:
a = 4, 8
b = 4, 2
c = 2, 3
Kuakisi abc kwenye ‘mstari wa kioo’ wima (x=8) unatoa taswira (a1b1c1)
katika viwianishi vipya:
a1 = 12, 8
b1 = 12, 2
c1 = 14, 3
Angalizo
Kiolwa na taswira yake kwa kawaida huwa viko katika umbali sawa wa mstari wima (umbali unaopimwa katika pembe za kushoto) kutoka
kwenye mstari wa kioo, kwa mfano, kama ‘a’ ni mita 4 za mraba 4 kutoka kwenye mstari wa kioo, ‘a1’ lazima pia iwe mita 4 za mraba kutoka
kwenye mstari wa kioo.
Linganisha viwianishi vya x na y vya abc na a1b1c1 na zingatia kwamba mstari wa kioo wima unaacha viwianishi vya y bila kubadilika.
Vivyo hivyo, mstari wa kioo ulalo utaacha viwianishi vya x bila kubadilika.
Chanzo Asilia: BBC Schools, Website
Nyenzo-rejea ya 3: Uhamishaji