Nyenzo-rejea ya 3: Kiasi cha moyo
Taarifa za msingi/ welewa wa somo wa mwalimu
Kasi ya moyo ni neno linalotumika kuelezea kurudia rudia kwa mzunguko wa moyo. Kinasemekana kuwa ni moja kati ya alama muhimu nne. Kwa kawaida huhesabiwa kama idadi ya minyweo (mapigo ya moyo) ya moyo katika dakika moja na huelezewa kama ‘mapigo kwa sekunde’ (mks).
Akiwa amepumzika, kwa mtu mzima mapigo ya moyo huwa kama mks 70 (wanaume) na mks 75 (wanawake), lakini hii hutofautiana. Hata hivyo, kwa kawaida huwa kati ya 60 (kama ni chini ya hapo huitwa bradycardia [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)] ) na 100 mks (ikizidi huitwa tachycardia). Kiasi cha mapigo ya moyo katika hali ya utulivu chaweza kuwa chini kwa wakimbiaji. Kiasi cha mapigo ya moyo kwa watoto wachanga ni 130-150 mks, wanaotambaa ni 100-130 mks, wakubwa kidogo ni 90-110 mks na kijana ni 80- 100 mks.
Mwili unaweza kuongeza kiasi cha mapigo ya moyo kulingana na hali tofauti ili kuongeza msukumo wa moyo (kiasi cha damu kinachosukumwa na moyo kwa kizio kwa muda). Mazoezi, mfadhaiko wa kimazingira au kisaikolojia vinaweza kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka zaidi ya kiasi cha utulivu.
Kiasi cha mapigo ya mishipa (ambayo kwa watu wengi ni sawa na mapigo ya moyo) kinaweza kupimwa popote pale mwilini amabapo ateri iko
karibu na ngozi. Sehemu kama hizo ni kifundo cha mkono, shingo, kiwiko na kwenye kinena. Mapigo yanaweza pia kuhisiwa moja kwa moja kwenye eneo la moyo (kumbuka usitumie kidole gumba kupima kiasi cha mapigo, kwa kuwa vidole gumba vina mapigo yao vyenyewe).
Pia inawezekana kupima kiasi cha mapigo ya moyo kwa sauti, kwa kusikiliza sauti zinazotokana na moyo wakati unapiga. Sauti hizi zinaweza kusikilizwa kwa kutumia stetoskopu (chombo cha kusikilizia mapigo ya moyo)
Nyenzo-rejea ya 2: Namna gani ramani za mawazo zinaweza kuwasaidia waalimu na wanafunzi wa hisabati