Somo la 1
Utangulizi mzuri wa kutaja muda ni kujadili kwanza njia anuwai watu walizotumia kutaja muda kabla ya kugundulika kwa saa. Unaweza kuwauliza wanafunzi wako namna wanavyofikiri wangeweza kutaja muda leo, bila kutumia saa. Kuchunguza dhana hizi kwanza na kusikiliza majibu yao kutakupa ushahidi wa uelewa wao wa sasa. Hii itakusaidia kuhakiki jinsi gani wamejifunza baada ya baadhi ya shughuli kuhusu muda.
Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza njia zilizotumika kutaja muda
Bi Tokunbo ni mwalimu wa shule ya msingi iliyoko Nigeria. Alipanga kufundisha ‘kutaja muda’ kwa wanafunzi wake. Alitaka kuanza kwa kuwasaidia wote waelewe uhitaji wa njia sanifu ya kutaja muda.
Kwanza, aliwataka wamwambie walifikiri nini kuhusu namna ya kutaja muda na aliorodhesha mawazo yao ubaoni. Alijadili njia nyingine za kutaja muda za zamani, zikiwa ni pamoja na mishumaa yenye alama, shisha na saa za vivuli. Kwa kila moja ya njia hizi za kutaja muda, aliwataka wanafunzi wafikiri ingekuwa vipi kutegemea njia hiyo, na ingeweza kusababisha matatizo gani. (Angalia Nyenzo rejea 1: Njia za kupima muda za zamani kwa mifano ya nini Bibi Tokunbo aliwaambia wanafunzi wake.)
Shughuli ya 1: Kujadili namna ya kutaja muda kwenye makundi
Anza somo lako kwa kuwataka wanafunzi wako wafikiri njia ambazo watu hutaja muda bila kutumia saa na andika mawazo yao ubaoni. Unaweza hitajika upendekeze baadhi ya mifano, kama vile kuchomoza na kutua kwa jua, kufunguka na kujifunga kwa maua kama Etinkanika, au mifano kwenye Nyenzo rejea 1, Nyenzo rejea 2: saa za maji na Nyenzo rejea 3: saa zavivuli ).
Wapange wanafunzi kwenye makundi ya watu wanne au watano na waulize wanajuaaje muda wa siku unavyokuwa. Halafu waambie wajadili jinsi wanavyofikiri hizi njia zinafaa. Yaambie makundi yatoe mrejesho na kuwe na majadiliano ya darasa, ukiandika maoni yanayofaa, ya njia sahihi za kutaja muda.
Sehemu ya 2: Kupima na kusimamia muda