Somo la 2
Kukusanya data ni sehemu tu ya utafiti, data zinahitaji kuchunguzwa na kuwasilishwa ili ziweze kueleweka na kushirikishwa kwa wengine. Wanafunzi wanaweza kuwasilisha data zao kwa picha,chati duara,grafu za michirizi, grafu za mistari. Ni muhimu wanafunzi waelewe kielelezo husika kwa kila aina ya data, hiyvo mifano yako lazima iwe wazi. Maelezo mafupi kwa kila kielelezo yametolewa kwenye Nyenzo - rejea 2: Chati na Grafu
Tumia data zinazotokana na mazingira halisi ya wanafunzi, hata hivyo ni wazo zuri pia kutumia mifano kutoka kwenye magazeti, majarida na machapisho ya Serekali.Inachukua muda kuwawezesha wanafunzi kuelewa matumizi ya vielelezo mbalimbali. Wapangie shughuli mbalimbali za kufanya kwa kila kielelezo ili kuimarisha ufahamu wao.
Uchunguzi kifani ya 2: Kuchora Chati
Baada ya kukusanya data, Mwalimu Msemakweli alitaka wanafunzi wake waamue jinsi watakavyowasilisha data walizokuwa wamekusanya.
Alileta darasani mifano aliyokuwa ameikusanya kutoka kwenye magazeti, majarida na nyaraka za serikali, lakini akachagua mifano mitatu tu ya chati ya kuwaonyesha. Alikuwa na mifano ya takwimu za wanafunzi na shule kutoka Ofisi ya Elimu, na alijua kuwa hizo zilikuwa na maana kubwa kwa darasa. Wanafunzi walikuwa na uzoefu wa mwaka mmoja kwa aina zote tatu za Chati, na hivi Mwalimu Msemakweli ilibidi awakumbushe tu jinsi ya kuzitumia.
Baada ya majadiliano ya darasani juu ya njia zilizokuwa zimetumika kuwasilisha takwimu, aliwaagiza wanafunzi warudi kwenye makundi yao
kujadiliana juu ya njia bora zaidi za kuwasilisha data hizo. Wengi walitaka kutumia chati ya michirizo (angalia Nyenzo - rejea 2 ) aliwasaidia wakati kila kundi likichora chati yake. Mwishowe walionyeshana matokeo ya kazi hiyo
Mwalimu Msemakweli aliona njia hii inapendelewa zaidi na wanafunzi kwani licha ya kuwashirikisha pia inawawezesha kumiliki yale wanayogundua.
(Angalia Nyenzo Rejea Muhimu: Kutumia kazi ya kundi darasani.)
Shughuli ya 2: Kuwasilisha data
Kabla ya kipindi hiki, tumia Nyenzo - rejea 2 kuelewa aina mbalimbali za chati, matumizi yake na vipengele muhimu vya kujifunza kwa kila aina ya chati.
Kusanya mifano ya data zinazowasilishwa kwa chati mduara, picha, chati mchirizi, grafu ya msitari; waonyeshe wanafunzi ili waweze kuona umuhimu wa kuchagua chati sahihi. Tumia muda wa kutosha kufafanua aina ya taarifa inayowasilishwa kwenye kila chati.
Panga mfululizo wa vipindi kwa ajili ya kufundisha jinsi ya kutengeneza kila aina ya chati na jinsi ya kutumia stadi hizo. Kwa kila aina ya chati, fikiria chanzo cha data zitakazokusanywa na wanafunzi, na jinsi utakavyowasaidia wanapotengeneza chati zao. Mambo wanayoweza kuchunguza katika jumii yao ni pamoja na umuhimu wa kujenga shule nyingine au Kituo cha Afya.
Somo la 1